Na Magreth Mbinga
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa amekipongeza Chuo Kikuu h
Huria cha Tanzania kupitia kitengo cha teknolojia kwa kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu kufikia malengo yao ambayo wanatarajia.
Hayo ameyazungumza leo katika ufunguzi wa maonesho ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yanayo ratibiwa na kusimamiwa na Tume za Vyuo Vikuu Nchini (TCU) baada ya kutembelea banda la Chuo hiko na kukutana na mwanafunzi Barnadetha Msigwa mwenye ulemavu wa macho ambae ameweza kuandika kitabu.
Aidha Mh Majaliwa ameweza kushuhudia namna Bernadetha anavyoweza kutumia vifaa vya teknolojia kwa ufanisi mkubwa katika kufanya kazi zake hivyo ametoa agizo kuwa Msigwa achukuliwe taarifa zake kwaajili ya kuangalia namna anaaeza kupata nafasi ya utumishi ili aweze kutoa ujuzi kwa manufaa ya Taifa.
Maoneaho hayo ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yanayo ratibiwa na kusimamiwa na Tume za Vyuo Vikuu Nchini (TCU) yamefanya Chuo Kikuu Huria kuwa chuo pekee ambacho kimeweza kushirikisha wanafunzi wenye ulemavu kuonesha kazi zao za kitaaluma .