Home Kitaifa RC KINDAMBA: NIMEFURAHISHWA NA UWEKEZAJI WA STEM PARK

RC KINDAMBA: NIMEFURAHISHWA NA UWEKEZAJI WA STEM PARK

Na Boniface Gideon, TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameonesha kufurahishwa na uwekezaji mkubwa wa Kituo Cha Sayansi mkoani Tanga Cha STEM PARK kilicho chini ya usimamizi wa Project Inspire kwakushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na Wadau wa Maendeleo.

Akizungumza Jana Wakati wa ziara yake ya kukagua Miradi ya Tanga Yetu ambayo inasimamia Miradi 17 katika Mkoa wa Tanga ikiwamo Ujenzi wa mradi wa Bustani ya kisasa ya mapumziko Jijini Tanga maarufu Forodhani,Kituo Cha Sayansi Cha STEM PARK pamoja na mradi wa ugaji Kuku na ufugaji Majongoo Bahari.

Kindamba Alisema uwekezaji huo mkubwa wa Kituo Cha Sayansi utausaidia Mkoa wa Tanga kuzarisha Wanasayansi mahiri ambao watakuja kulisaidia Taifa hapo baadae,

“Uwekezaji huu mkubwa wa Kituo Cha Sayansi mkoani kwetu utatusaidia kupata wataalamu Wengi hapo mbeleni na kiukweli nimefurahishwa Sana na kitu kikubwa kama hiki kuwepo mkoani Tanga” Alisema Kindamba

Alisema Serikali imeweka Mazingira wezeshi ya Elimu kwakuhakikisha kila Mtoto anapata Elimu bila vikwazo nakuwataka Wazazi kuhakikisha wanawapatia Watoto wao Haki yao ya kupata Elimu,

“Serikali imeweka Mazingira wezeshi ya Elimu, hivyo niwaombe Wazazi,walezi wahakikishe Watoto wanapata Elimu lakini pia wakitumie Kituo hiki ili tupate Wanasayansi mahiri wa baadae” Alisema Kindamba

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!