Home Kitaifa ASKOFU DAO: MABADILIKO YATUFANYE KUINUKA KIUCHUMI NA KUFANYA IBADA

ASKOFU DAO: MABADILIKO YATUFANYE KUINUKA KIUCHUMI NA KUFANYA IBADA

Na Shomari Binda-Musoma

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC) maarufu Bonde la Baraka,Daniel Ouma,amesema ni muhimu kufanya mabadiliko ili kujiinua kiuchumi.

Mabadiliko hayo ni pamoja na kuacha pombe na kufanya kazi kwa bidii mara baada ya kushiriki ibada mbalimbali za kumuomba Mungu.

Ujumbe huo ameutoa leo kwenye ibada ya jumapili iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu lililopo Kigera bondeni manispaa ya Musoma mjini.

Amesema mabadiliko yanaanza ndani ya moyo kwa kuachana na mambo yasiyofaa na yanayokatazwa na Mungu na kushika mambo mema.

Askofu huyo maarufu kama askofu Dao,amesema mabadiliko ni jambo la muhimu na kudai Yesu alikuja kwaajili ya mabadiliko ya mwanadamu.

Amesema unywaji wa pombe za kupindukia na kushindwa kufanya kazi huwezi kuwa na uchumi hivyo mabadiliko yanatakiwa kwa kila mmoja.

Dao amesema yapo mabadiliko ambayo yanahitajika kwenye maeneo mengi ili kupata maarifa yakufanya mambo yanayofaa.

Amesema hata mtoto mdogo anakuwa katika mabadiliko yakiwemo ya ukuaji ambayo Mungu amekuwa akimsimamia katika ukuaji wake.

“Kuna siku nimemsikia mkuu wa mkoa wa Mara akisema mkoa umefanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha 6 na hayo ni mabadiliko makubwa”

Ni muhimu kufanya ibada na sala mbalimbali lakini ni muhimu pia kufanya kazi ili kuwa na kipato kitakachotusaidia na kuwa na mabadiliko kwenye jamii zetu” amesema askofu Dao.

Mmoja wa wageni katika.Kanisa hilo,James Peter,amesema Kanisa la bonde la bonde la baraka linaye Askofu ambaye ni mwalimu mfundishaji anayetoa somo linalojenga jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!