Home Kitaifa Vikundi vya mchakamchaka vyatakiwa kuzingatia Sheria za Usalama barabarani

Vikundi vya mchakamchaka vyatakiwa kuzingatia Sheria za Usalama barabarani

VIKUNDI vya mazoezi ya mchakamchaka Jijini Mwanza wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuwawezesha kufahamu mambo wanayotakiwa kuzingatia nyakati watumiapo njia hizo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amewataka wakimbia mchakamchaka wanapokimbia kutokuvuka njia za waenda kwa miguu kwenye barabara ili kuepuka ajali.

Aliwataka wakimbiapo barabarani kuvaa nguo zinazoakisi mwanga ili kuwezesha madreva wa vyombo vya moto kuwaoana vizuri.

Tunaomba msajili vikundi vyenu kwenye halmshauri zenu ili mweze kutambulika”alisema Mtafungwa.

Nguo zinazoshauliwa kuvaliwa katika nyakati hizo ni zile za rangi ya kijani na manjano kwa kuwa na uwezo wa kuakisi mwanga kwa urahisi.

Alisema jeshi hilo litatoa ushirikiano kwa vikundi vya mchakamchaka vifanyapo mazoezi barabarani ili kuwezesha usalama wao wanapotoa taarifa kwao kuhusiana na kusudio la kufanya mazoezi.

Naye Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoani Mwanza (RTO) Sunday Ibrahim alisema kuwa wataendelea kutoa elimu mara kwa mara ili kuwezesha watu wengi kupata ufahamu juu ya vitu vya kuzingatia wanapofanya mazoezi kwa kupitia kwenye barabara.

Aliwataka kuepuka uvunjifu wa Sheria za Usalama barabarani kwa kuzingatia kuvaa nguo zenye kuakisi mwanga na kutoa taarifa mapema kwao wanapokuwa na uhitaji wa kufanya mazoezi kwenye barabara ili waweze kuwapa ulinzi.

Kamanda Ibrahim amesema kuwa askari wa Usalama barabarani watatoa ushirikiano kwa vikundi hivyo ili kuwezesha usalama wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!