Home Kitaifa CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) KIKUBWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) KIKUBWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Na Magreth Mbinga

Mkurugenzi wa shahada za awali Dodoma (UDOM) Dk Victor George Marealle amesema chuo hicho ni kikubwa Afrika Mashariki na Kati kilianza mwaka 2007 ambacho kina wanafunzi 82,000 ambao wamegawanyika katika stashahada,shahada za awali, shahada za umahiri na shahada uzamivu.

Hayo ameyazungumza katika mahojiano na mwandishi wetu wakati wa ufunguzi wa maonesho ya vyuo vikuu ambayo yameandaliwa na TCU na kusema kuwa chuo hiko kina taasisi mbili,shule kuu tatu,ndaki (colleges)sita,kuna shule kuu ya sheria,shule kuu ya uuguzi na shule kuu ya udaktari.

Tuna taasisi ya lugha na taasisi ya taaluma za maendeleo ambayo kwa ujumla tunatengeneza ambazo kwa pamoja tunatengeneza umoja wa taaluma umoja huo unatengeneza shahada za taaluma tofauti tofauti” amesema Dkt. Marealle

Aidha Dk Marealle amesema kuna jumla shahada za awali themanini ambazo zimetawanyika katika maeneo ya udaktari, uuguzi, sayansi asilia, sheria, uongozi, uchumi na biashara, TEHAMA na sayansi ya ardhi pia kuna shahada za juu hamsini na tatu.

Katika chuo chetu kuna maktaba za kisasa katika kila chuo cha kati ambapo mwanafunzi atapata vitabu vya kutosha na chuo chetu kimejengwa kisasa ambacho kinaweza kuhudumia wanafunzi elfu arobaini katika huduma ya malazi” amesema Dkt. Marealle

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!