Home Kitaifa CHONGOLO KUFANYA MKUTANO WA HADHARA JULAI 29,2023 DAR ES SALAAM

CHONGOLO KUFANYA MKUTANO WA HADHARA JULAI 29,2023 DAR ES SALAAM

Na Magrethy Katengu

CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es salaam wanatarajia kufanya Mkutano Mkubwa wa hadhara Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Julai 29 mwaka huu lengo kuelezea wananchi Mafanikio yaliyofanyika kupitia chama Tawala .

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CCM Mkoa Abbas Mtemvu amesema Siku hiyo wataenda kuwaeleza wananchi namna Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassani alivyowezesha kazi kubwa kufanyika katika sekta ya Afya, Elimu, barabara, Maji, Umeme, biashara, na uwezeshaji wananchi kiuchumi .

“Katika siku hiyo sisi tuna kila sababu ya kushukuru matunda haya yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika kusatawisha Jiji letu la Dar es salaam hivyo wananchi karibuni mtapata fursa ya kusikia mengi na kuuliza maswali yenu na kujibiwa,” amesema Abasi Mtemvu

Hata hivyo Mkutano huo utajumuisha burudani za makundi ya wasanii pia kutakua na fursa kwa wajasriamali wadogowadogo na kufanya biashara

Aidha katika Mkutano huo mkubwa wa hadhara Katibu Mkuu wa CCM Komredi Daniel Chongolo anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi atakayeongea na wananchi hivyo wananchi wote wa mkoa , makundi yote , jinsia zote, wanachama na ambao siyo wanachama kutoka wilaya zote tano kuhudhuria kwani mkutano utaanza saa 3;00 asubuhi siku ya Jumamosi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!