Home Kitaifa MAKAMU MWENYEKITI CCM TAIFA,ABDULRAHAMAN KINANA KUWASILI MARA KESHO

MAKAMU MWENYEKITI CCM TAIFA,ABDULRAHAMAN KINANA KUWASILI MARA KESHO

Na Shomari Binda-Musoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahaman Kinana, anatarajiwa kuwasili mkoani Mara kesho kufanya ziara ya siku moja.

Akizungumza ofisini kwake, Katibu wa CCM mkoa wa Mara,Langaeli Akyoo,amesema maandalizi ya mapokezi ya kiongozi huyo yamekamilika.

Amesema kiongozi huyo atapokelewa wilayani Bunda na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo na mkoa na kuelekea mjini Musoma kwaajili ya mapumziko

Akyoo amesema akiwa mkoani Mara,Kinana ambaye ataongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho,Sophia Mjema na viongozi mbalimbali atafanya mkutano wa hadhara shule ya msingi Mukendo julai 26.

Amesema kabla ya mkutano wa hadhara ataweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa ukumbi wa mikutano unaojengwa na chama hicho mjini Musoma.

Katibu huyo amesema baada ya kuweka jiwe la msingi atahudhulia na kuzungumza kwenye kikao cha halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mara

Tunao ugeni Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mara wa Makamu Mwenyekiti Taifa Comred Abdulrahman Kinana ambaye atawasili kesho.

Maandalizi ya mapokezi ya kiongozi wetu yamekamilika na atapokelewa kule wilayani Bunda na atakuwa na ziara ya siku moja“, amesema Akyoo.

Kufuatia ugeni huo Akyoo amewaomba wanachama na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kuhudhulia kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika shule ya msingi Mukendo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!