Home Afya DAWA ASILIMIA 100 ZAPATIKANA ZAHANATI YA NYAKATO JIMBO LA MUSOMA MJINI

DAWA ASILIMIA 100 ZAPATIKANA ZAHANATI YA NYAKATO JIMBO LA MUSOMA MJINI

Na Shomari Binda-Musoma

UPATIKANAJI wa dawa na vifaa tiba kwa ngazi ya zahanati vimeelezwa kupatikana Kata ya Nyakato jimbo la Musoma mjini kwaajili ya huduma za afya.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara uliofanyika Kata ya Nyakato.

Amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha nyingi kwaajili ya huduma za afya.

Mathayo amesema suala la afya ni jambo la msingi na kila anapoomba fedha serikalini kwaajili ya shughuli za jamii amekuwa akipatiwa.

“Leo nimeanza mkutano wangu wa kwanza kuzunguka Kata 16 za jimbo letu kuzungumzia masuala mbalimbali na nimeanzia hapa Nyakato na suala la huduma za afya ziko vizuri na huduma nyingine”

“Daktari wetu wa zahanati amesema upatikaji wa dawa na vifaa tiba ni kwa asilimia 100 na mimi bado nitaendelea kufatilia pale kwenye mapungufu”, amesema Mathayo.

Amesema licha ya huduma za afya lakini pia huduma nyingine za kijamii zikiwemo elimu,maji na miundombinu ya Barabara zimekuwa zikipitika wakati wote.

Mbunge huyo amesema kazi iliyobaki ni kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi na vyanzo mbalimbali ili kumudu maisha.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Nyakato, Joseph Tikina amemshukuru mbunge Mathayo kwa jitihada zake za ufatiliaji wa masuala mbalimbali ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!