Home Kitaifa BENKI YA TCB YAKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI SHULE MSINGI MASIWANI...

BENKI YA TCB YAKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI SHULE MSINGI MASIWANI TANGA

NA BONIFACE GIDEON, TANGA

BENKI ya Taifa ya Biashara (Tanzania Commercial Bank) leo imekabidhi Vifaa vya vya Ujenzi katika Shule ya Msingi Masiwani iliyopo kata ya Majengo Jijini Tanga. Vifaa hivyo ni pamoja na Mifuko ya Saruji 100 na Mabati 100 kwaajili ya kuezekea .

Akikabidhi msaada huo Meneja wa Benki hiyo Tawi la Tanga Patrick Swenya alisema Msaada huo ni Sehemu ya kurejesha fadhira kwa Jamii inayotokana na huduma za Benki hiyo,

“Tulipokea maombi kutoka utawala juu ya kuisaidia Shule hii Kongwe na sisi tulilifanyia kazi na Leo tumeleta msaada huu ambao utasaidia kufanya ukarabati wa Majengo ya Shule hii” Alisema Swenya

Aliongeza kuwa Vifaa hivyo vinathamani ya Mil 5,
Msaada huu unathamani ya Mil.5 lakini pia tutaendelea kutoa msaada zaidi ya hapa ,Benki yetu ni ya Serikali hivyo tutaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwaletea Wananchi Maendeleo” Alisema Swenya

Akipokea msaada huo Mkuu wa ya Wilaya Tanga James Kaji aliishukuru Benki hiyo kwa msaada huo nakuutaka uongozi wa Shule hiyo kuutumia vizuri,

“Naomba msaada huu utumike kwenye malengo yaliyopangwa , Mdau amejitolea kusaidia ni lazima aone matokeo chanya ya kile alichokitoa , nataka ukarabati uanze Mara moja lakini pia Ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo fedha zake zipo Tayari uanze Mara moja” Alisisitiza Kaji

Kwaupande wake Diwani wa kata hiyo Said Perembo alisema Shule hiyo inazaidi ya Miaka 80 na Majengo yake ni mabovu kupita kawaida hivyo Wadau wanahitajika zaidi ili kuipata hadhi mpya Shule hiyo,

Hii Shule ni Kongwe kuliko Simba na Yanga na imechakaa Sana hivyo juhudi nyingi zaidi kutoka Serikalini na Wadau mbalimbali zinahitajika kwaajili ya kuikarabati Shule hii Kongwe na kujenga vyumba vipya vya madarasa” Alisisitiza Perembo

Alisema kuwa kata yake inauhaba wa Shule ya Sekondari nakuiomba Serikali kufikiria kujenga,

“Kata yetu haina Sekondari hivyo tunaomba mambo mawili aidha Serikali ifanye mazungumzo na TBA ili watupatie eneo lao ambalo lipo wazi halifanyiwi shughuli zozote au tuibadilishe Shule hii Kongwe iwe Sekondari kwakuwa eneo hili linashule mbili za Msingi katika eneo moja na zote hazina idadi kubwa ya Wanafunzi” Alisisitiza Perembo

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!