Home Kitaifa TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 6 WA WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA WA AU

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 6 WA WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA WA AU

Na. Joseph Mahumi, Nairobi. 

Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 6 wa Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Kikao hicho kinafanyika tarehe 17 hadi 19 Julai 2023, katika ukumbi wa hoteli ya Movenpick, jijini Nairobi, nchini Kenya. 

Kikao hicho kimelenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo. 

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao mbalimbali ambavyo Serikali ya Tanzania imekua ikishiriki ili kutafuta fursa mbalimbali zitakazosaidia ukuaji wa uchumi imara wa nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!