Na Theophilida Felician Kagera.
Serikali ya Mkoa Kagera imeeleza kuwaunga mkono wadau wamichezo mkoani humo ili kuinua juu kiwango cha vipaji vya michezo kwa wananchi kuanzia ngazi ya watoto shuleni, vijana na kuendelea
Ameyasema hayo Afisa elimu wa Mkoa Kagera mwalimu Khalifa Shemahonge kwenye tamasha la mchezo wa ngumi viwanja vya Muyunga lilioandaliwa na Taasisi inayojihusisha na mchezo wa mpira wa miguu sambamba na mchezo wa ngumi (ZAAGWA )Manispaa ya Bukoba.
Shemahonge akiwa Mgeni rasmi wa tamasha hilo kwa niaba ya Katibu tawala wa Mkoa Kagera Toba Nguvila amesema kuwa Kagera ina histori ya kimichezo tangu miaka ya nyuma kwani imewahi kutoa wachezaji kwenye timu za Taifa na kadharika.
Ameendelea kutoa ufafanuzi kuwa juhudi za kukuza michezo Kagera zinapaswa kuanzia shuleni jambo ambalo litachochea kuviibua vipaji mbalimbali kwa watoto wadogo hadi watu wazima.
Ameipongeza taasisi ya (ZAAGWA) chini ya Mkurugenzi wake Walesi Lugakingira kwa kitu kikubwa ilichokifanya kuandaa tamasha la mashindano ya ngumi katika mji wa Bukoba.
“Sisi Kagera hapa tunahitaji sana watu kama hawa na kuwapa moyo kwa hiyo kwa niaba ya Serikali nasema kwamba Serikali iko tayari kuweza kutoa kila aina ya uungwaji mkono kama mnavyojua kila mmoja alivyo shahidi Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassani ni mpenzi mkubwa sana wa michezo na hivyo michezo ameipa joto kweli kweli hapa nchini kama mlivyoona timu zetu za kitaifa zilivyoshiriki mashindano ya kimataifa alikuwa mstali wa mbele usiku na mchana kwa ajili kutoa ushirikiano hatimaye tukapata mafanikio makubwa na kulitangaza taifa” Amesisitiza Afisa Khalifa.
Ameongeza kusema kuwa vipaji walivyonavyo vijana wadogo wa Mkoa Kagera ni dalili njema kuwa miaka ijayo Mkoa Kagera utaweza kupata watu imara katika sekta ya michezo ikiwemo mchezo wa ngumi.
“Kuna akina Mandonga hapa akina Mwakinyo watatoka hapa kwa hiyo Sina shaka kwamba tukiendelea na matamasha kama haya kwakweli yatakuwa yanalipa Mkoa utakuwa katika nafasi nzuri kimichezo nitowe wito kwa wadau wengine kama ZAAGWA tuunge mkono jitihada hizi za Serikali na wadau kama bwana ZAAGWA kuweza kuandaa matamasha mengine ya michezo kama haya, kuwepo kwa michezo hii watu wanapenda sana kwani wanapata burudani ambayo ni salama kama tunavyoshuhudia watu walivyojazana hapa kwa ajili ya kupata burudani hii ya ngumi” amefafanu kwa kina Khalifa Shemahonge
Mratibu Mkuu wa mashindano ya mchezo huo Robati Kyaluzi ameeleza kuwa mchezo wa mapambano ya ngumi uliowakutanisha mabondia kutoka Mkoani Mwanza na waenyeji Bukoba umefana vizuri kwa washiriki pande zote wameonyesha uwezo mkubwa wenye kuwatia moyo wao kama wandaaji jambo ambalo ni lakujivuni haswa.
Robati amesema kwamba jumla ya mabondia (24) wameshiriki mchezo huo ambapo ameahidi kuwa mabondia kutoka Bukoba wanaenda kujipanga upya ili kuziba walipo yumba ndani ya mtanange huo.
Ameahidi kuwa wao kama wandaaji timu ya vijana ya Bukoba wanaenda kuisuka zaidi ili kuweza kuwaibua wachezaji wakubwa wa mchezo huo kitaifa na kimataifa.
Kwa upande wao mabondia wa Bukoba wamesema kuwa wana matamanio makubwa ya kufika mbali kupitia mchezo wa ngumi hivyo wameiomba serikali kuwaunga mkono zaidi ili waweze kufanya kitu kikubwa na chenye mageuzi ya michezo hususani kuandaa mashindo ya ngumi mara kwa mara.
Mwalimu wa mabondia wa ngumi Mkoa Kagera Nuru sadick Omuyaya Tafa amesema kuwa vijana wa kagera wamecheza vizuri katika mchezo huo licha kupoteza nafasi nyingi kiushindi kuna sababu mbalimbali ziliwapelekea hali hiyo.
“Labda nigusie kidonda chenyewe ZAAGWA imeangalia mbali mno kimkoa kitaifa na kidunia mkoa wa Kagera Ngumi zipo sema tuu ngumi bila Serikali kuweka mkono ngumi hufanikiwi kamwe Mhe Rais mama Samia anakipenda kitu hiki Kagera uongozi utuunge mkono kuanzia uongozi wa chini mpaka wa juu tutafanikiwa kwa kishindo mchezo wa namna hii” Ameeleza Mwalimu Nuru.
Mashindano ya mchezo wa ngumi yameonekana kuwavutia wananchi wengi wa mji wa Bukoba baada kujitokeza kwa wingi na kushudia kandanda ya mchezo huo ambapo wachejizaji kutoka Mkoa wa Mkoa wa Mwanza weamfanikiwa bakubwa ushindi dhidi ya wenzao wa Bukoba.