Home Kitaifa MWENYEKITI WA ALAT TAIFA AREJEA KWA KISHINDO AANZA MAJUKUMU RASMI BAADA KUKUTWA...

MWENYEKITI WA ALAT TAIFA AREJEA KWA KISHINDO AANZA MAJUKUMU RASMI BAADA KUKUTWA NA AJALI ILIYOMPELEKEA KUKATWA MGUU.

Na Theophilida Felician Kagera.

Mwenyekiti wa ALAT Taifa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe Murshid Ngeze amerejea tena kuanza utekelezaji wa usimamizi wa shughuli za Halmashauri ya Bukoba baada yakutokuwepo kazini kwa muda murefu kutokana na tatizo la ajali iliyomkuta na kusababisha kukatwa mguu wake wa kulia.

Akizungumza baada ya kuanza shughuli za ukuitembelea miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa katika Halmashauri hiyo amesema kwamba baada yakufika kutoka kwenye matibabu kwamuda wa miezi saba amesema kuwa amepokea taarifa ya ujio wa fedha zaidi ya Bilioni moja (1) tangu mwezi January zilizotoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Amefafanua kuwa awali ameanza kuitembelea miradi miwili ambayo ni maendeleo ya ukamilishaji wa ujenzi wa majengo mapya ya Halmashauri pamoja na ujenzi wa shule ya Kazi B sambamba na ukarabati wa shule moja kongwe Kanazi A iliyojengwa mnamo mwaka wa (1926 )

Ameeleza kuwa amekuta jengo la Halmashauri likiwa ukingoni kukamilika kwani baadhi ya nyumba zimekamilika ikiwemo ya Mkurugenzi.

Nimeona kweli ujenzi umeenda vizuri safi sana kabisa tumekubaliana na Mkurugenzi kwamba mwezi wa nane kabla ya Tarehe 30 ya mwezi wa nane tuwe tumehamia mule” amesema Murshid Ngeze.

Hata hivyo ameongeza kusema kuwa zimetolewa zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Kanazi B pamoja na zaidi ya milioni 90 ya ukarabati wa shule kongwe Kanazi A ambayo ilikuwa na hali mbaya ya kuchakaa.

Mwenyekiti Ngeze ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa jinsi inavyojizatiti kwa nguvu zote katika kuhakikisha inafanya juu chini na kutoa fedha za kujenga miradi yamaendeleo ya wananchi wakiwemo wa Bukoba huku akitoa wito kwa wananchi kuilinda na kuitunza miundo mbinu ya miradi ya maendeleo ili iweze kudumu na kuwasaidia kwa kipindi kirefu.

Mwenyekiti huyo akiambatana na mkurugenzi wa Halmashuri ya Bukoba Fatna Laay wametembelea miradi hiyo nakushuhudia kazi kubwa ya ujenzi inavyozidi kufanyika kwa kasi zaidi inayochochea miradi hiyo kukamilika mapema na kuanza kutumika hususani madarasa ya wanafunzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!