Home Kitaifa MCHANGO WA MBUNGE MUHONGO WATAMBULIWA UJENZI WA SEKONDARI MPYA YA BWAI

MCHANGO WA MBUNGE MUHONGO WATAMBULIWA UJENZI WA SEKONDARI MPYA YA BWAI

Na Shomari Binda-Musoma

MCHANGO wa mbunge wa jimbo la Musoma vijijini,Prof.Sospeter Muhongo, katika sekta ya elimu umetambuliwa na kupongezwa kwa juhudi zake.

Katika taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge,Abdara Shaibu,iliyotolewa na mkuu wa shule mpya ya sekondari ya Bwai iliyotolewa na mkuu wa shule hiyo,Rozalia Laurent,amesema Muhongo amekuwa mmoja wa hamasa kubwa ya ujenzi.

Amesema hadi kufikia sasa amechangia fedha yake shilingi milioni 7,241,500,00,mfuko wa jimbo milioni 18,010,000,00 na mchango wa wadau wengine milioni 6963,500,00.

Mkuu huyo wa shule amesema mradi huo umeondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mtefu kwenda shuleni na kuondoa tatizo la utoro.

Amesema shule ya sekondari Bwai iliyosajiliwa novemba 2022 kwa naomba S.5996 ni ya kutwa na ina jumla ya wanafunzi 138 wa kidato cha kwanza pekee.

Akitoa salami za mbunge huyo,mkuu wa wilaya ya Musoma,Dk.Khalfan Haule,amesema Prof.Muhongo alitamani kuwepo kwenye tukio la mwenge lakini yapo majukumu ya kitaifa anayoyatekeleza.

Amesema suala la elimu ndio kipaumbele kikubwa kwa Muhongo na amekuwa akichangia kwenye shule mbalimbali zikiwa za msingi na sekondari.

Tungekuwa hapa na mheshimiwa mbunge lakini anayo.majukumu ya kitaifa na kaniomba nimfikishie salamu zake na licha ya mambo mengine ametuchangia chakula“,amesema.

Akisoma risala ya utii,mkuu huyo wa wilaya amesema mwenge wa uhuru umetembelea miradi 7 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ukiwemo uwekaji wa jiwe la msingi shule mpya ya sekondari Bwai.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Abdara Shaibu,amesema serikali inaendelea kuwajali wananchi kwa kuhakikisha wanapata elimu stahiki na maeneo jirani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!