Home Kitaifa KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ARIDHISHWA NA MRADI WA MAJI ULIOTEKELEZWA NA...

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ARIDHISHWA NA MRADI WA MAJI ULIOTEKELEZWA NA MUWASA

NA Shomari Binda-Musoma

KIONGOZI wa mbio za mwenge,Abdara Shaibu ameridhishwa na mradi wa maji uliotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA).

Hayo ameyasema leo mara baada ya mwenge wa Uhuru kufika eneo la Nyabisare kukagua na kuangalia mradi wa maji katika moja ya mitaa ya pembezoni ya manispaa ya Musoma iliyokuwa haina huduma ya maji.

Amesema baada ya kutembelea mradi huo na kuangalia nyaraka mbalimbali amejiridhisha bila shaka utekelezaji wake.

Shaibu amesema lengo la serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kumtua mama ndoo kichwani na MUWASA inafanya kazi nzuri kwenye majukumu yao.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo,mkurugenzi mtendaji wa Muwasa,Nicas Mugisha,amesema utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji kwenye mitaa 7 iliyokuwa haina huduma ya maji ulianza juni 15 mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika juni 30 mwaka 2024.

Amesema utekelezaji wa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 709 ambapo fedha zote ni kutoka serikali kuu na utahudumia watu elfu 40.

Nicas amesema kwa niaba ya wananchi wanaishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na sslama katika manispaa ya Musoma.

Kwa upande wske mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2020 waliahidi kufikisha maji maeneo yote ya jimbo na wanakwenda kukamilisha kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Amesema sio sekta ya maji pekee serikali inakwenda kutekeleza miradi mbalimbali iliyopo kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Khalfan Haule amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kupokea mwenge wa Uhuru unaokimbizwa kwa kilometa 50 na kutembelea miradi 7.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!