Home Kitaifa EPZA YAONESHA FURSA KATIKA SEKTA YA KILIMO KWA KUYAONGEZEA THAMANI MAZAO

EPZA YAONESHA FURSA KATIKA SEKTA YA KILIMO KWA KUYAONGEZEA THAMANI MAZAO

Na Magrethy Katengu

Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje EPZA imekuwa Mstari wa mbele kuwaonesha fursa Wakulima kwa kuongeza mazao yao katika mnyororo wa thamani kupitia viwanda vikubwa, kati,na vidogo ili bidhaa zao zinazodhalishwa ziweze kuuzika kimataifa .

Akizungumza Jijini Dar es salaam Afisa Mhamasishaji Uwekezaji EPZA Nakadongo Fares amesema wao wamekuwa wakitoa leseni kwa viwanda vinavyozalisha kwa kuchukua malighafi ikiwemo kiwanda walochonacho cha Tiba lishe kuchukua mimea na kuvichakata kisha kusafirisha kwenda kuuza nje ya nchi

Hata hivyo amesema kiwanda hiko cha Tiba lishe kipo Bagamoyo kimekuwa kinawasaidia wananchi kwa kuwapatia mafunzo na kuchukua mimea yao na kuitengeneza kuiongezea thamani hivyo wananchi walipata fursa ya kujifunza teknolojia ya kisasa namna bora ya kulima

Hii ni fursa kubwa kupitia mwekezaji anayetaka kuwekeza kupitia kilimo kwani kuwepo kwa kiwanda hiki cha Tiba lishe kinatengezena fusa nyingi Nchi inapata kunakuwa na mnyororo kuanzia kwa wakulima kupata mafunzo kulima kilimo cha Organiki pasipo kuweka kemikali yeyote katika mimea mbalimbali ambayo waliwafundisha kisha kununua kutoka kwao na kuzalisha kisha kusafirisha kupeleka nje ya nchi” amesema Fares

Sanjari na hayo amesema Elimu ya teknolojia mpya liyokuwa ikotolewa inakwenda kwa wazawa wakulima na imewasaidia wenyewe kuboresha kulima kisasa zaidi kupitia teknolojia waliyoipata kwa kuboresha bidhaa zao baadae kusimama wenyewe kupitia kumiliki viwanda vidogo na vya kati kuzalisha bidhaa zap wenyewe kwenda nje ya nchi.

Na sisi Watanzania kupitia Wawekezaji hao tunapata fedha za kigeni kupitia viwanda kuuza bidhaa nje ya nchi na inasaidia kupunguza uingizwaji bidhaa za nje badala yake na sisi tunatoa kwenda kuuza na kutusaidia kujenga uchimi imara” amesema Fares

Aidha amesema EPZA ina Mfumo kiganjani wa kuhudumia Mto popote alipo pasipo kusafiri kwenda Ofisini kwa kila kitu wanafanya kupitia mtandao na wameweka mfumo huo ili kurahisisha uwekezaji na kujua fursa mabalimbali hivyo Wananchi mnakaribishwa kuja Banda la Sabasaba kupata elimu

Sambamba na hayo wamekuwa mstari wa mbele wakiwapatia elimu baadhi ya viongozi wa Mikoa ikiwemo Kigoma ,Mbeya kuhusu fursa zinazopatikana Mamlaka hiyo na kuwahamasisha kuandaa maeneo maalumu kwa ajili ya kuvutia uwekezaji wa viwanda ambavyo vitasaidia kuongeza thamani mazao yao kwa kujengea miundombinu ikiwemo barabara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!