Home Kitaifa VIKWAZO VYA UWEKEZAJI VIMEONDOLEWA KARIBUNI BANDA LA SABASABA EPZA MJIONEE FURSA

VIKWAZO VYA UWEKEZAJI VIMEONDOLEWA KARIBUNI BANDA LA SABASABA EPZA MJIONEE FURSA

Na Magrethy Katengu

Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje EPZA imesema serikali serikali iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani imeondoa kero zillzokuwa zinawafanya wawekezaji kukimbia hivyo inawakaribisha wale wenye nia ya kuwekeza kutembelea Banda la maonyesho sabasaba la EPZA kuona fursa zilozopo ikiwemo kilimo.

Akizungumza na Waandishi wa habari siku ya sikukuu ya Sabasaba Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Charles Ntembe amesema Serikali imetoa baadhi ya vikwazo ikiwemo nafuu ya tozo kumrahisishia mwekezaji wa ndani na nje ili naye avutike kuja kuwekeza kwani kupitia kufanya hivyo kunaleta tija kiuchumi kwa nchi..

EPZA tunatoa leseni kwa mwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje na tunaangalia na kutumia busara kwa mwekezaji anyeanza kutomtoza gharama kubwa kwani tunatambua mwelezaji anayeanza anahitaji mtaji hivyo lazima tuangalie na kukaa naye mezani kuzungumza naye kisha atoe gharama ambayo haitampelekea kufilisika na kukimbia” amesema Ntembe

Aidha amesema EPZA wamekuwa na jukumu la kusimamia kampuni zinazokuja kuwekeza kwa kiwaonyesha fursa zilozopo katika sekta mbalimbali ikiwemo katika madini, kilimo hivyo wale wote wanaohitaji kuwekeza wanaalikwa kupitia Mfumo wa EPZA kujihudumia popote walipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!