Home Kitaifa WATUHUMIWA 59 MBARONI MATUKIO YA KIHALIFU

WATUHUMIWA 59 MBARONI MATUKIO YA KIHALIFU

Na Magrethy Katengu

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es salaam linawashikilia Watuhumiwa 59 kwa makosa mbalimbali ikiwemo Unyang’anyi, kuvunja nyumba usiku na kuiba, uuzaji dawa za Kulevya.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Kamanda SACP Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika Operesheni Mbalimbali ilianzwa kufanywa Aprili 2023 katika maeneo mbalimbali ya Jiji na walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa 48 wa matukio ya unyang’anyi, uvunjaji nyumba usiku na walikamatwa ni Michaeli Jakobo(38) Mkazi wa Jeti Urumo, Hussein Rashid, (41) Mkazi wa Mtoni Mtongani, Mussa Mohamed(23) Mkazi wa Chanika

Operesheni kali maalum iliyoanza mwezi Aprili, 2023 na inayo endelea katika maeneo mbalimbali ya Jiji, imefanikiwa kuwanasa watuhumiwa sugu 48 wa matukio ya unyang’anyi na uvunjaji nyumba usiku na kuiba. Waliokamatwa ni Michael Jacob@ ngatunga (38) mkazi wa Jet lumo, Hossein Rashid (40) Mkazi wa Mtoni Mtongani na Mussa Mohamedi (23) mkazi wa Chanika, wote wa Dar es Salaam” Amesema SACP Muliro.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na vitu mbalimbali walivyoiba ikiwa ni pamoja na; laptop 24, simu za mkononi 59, Televisheni 31 za aina mbalimbali, mitungi 31 ya gesi ya ujazo wa kg 16, kamera 9 na subwoofer 2, Baadhi ya vitu vilivyo kamatwa tayari vimetambuliwa na wamiliki.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi pia limewakamata na linawahoji kwa kina watuhumiwa watano (5) kwa tuhuma za kupokea mali za kutoka kwa wezi hao na kuzifanya sehemu ya biashara zao.

Katika hatua nyingine, jitihada za kuzuia na kupambambana na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata muuzaji sugu wa bhangi Maneno Mayoge@ Bundala (28), mkazi wa Majimatitu, Mbagala, Temeke na wenzake wawili (2) wakiwa na bhangi gunia saba 07, puli 445, mbegu za bhangi kg 5 na magazeti ya kufungia bhangi wakiwa wezificha kwenye nyumba yao.

Pia Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 03 waporaji wa mikoba kwa pikipiki @vishandu. Pia imekamatwa Pikipiki namba MC. 252 DTG BOXER.

Aidha sikukuu ya Eid Alhaj, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanasherekea kwa amani na usalama umeimarishwa kwa kiwango cha juu katika maeneo yote ya ibada, maeneo ya fukwe na mitaani. Waendesha vyombo vya moto wanaendelea kutahadharishwa kufuata sheria na kujiepusha vileo wawapo na vyombo hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!