Na Magreth Mbinga
Bohari ya dawa MSD wametakiwa kuhakikisha dawa ambazo zinatolewa zifike vituoni na walio vitioni!! kuhakikisha zinawafikia wananchi ndio dhumuni la Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Uzazi Dkt. Felix Bundala wakati wa hafla ya kukabidhiwa bidhaa za uzazi wa mpango na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani UNFPA kwa niaba ya Wizara ya afya kukiwa na lengo la kuokoa vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Aidha Dkt. Bundala amesema afya ya mama na mtoto ni kipaumbele cha kwanza kwa Serikali cha 2020-2025 na kuhakikisha wanaajiri watoa huduma wenye weledi wanaotosheleza katika utoaji wa huduma.
Pia Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNFPA Tanzania Mark Bryan Schreiner amesema vifaa vya afya ya uzazi vilivyokabidhiwa na UNFPA kwa Serikali ya Tanzania ni bidhaa za kuokoa maisha ya uzazi zikiwemo bidhaa za kisasa za uzazi wa mpango .
“Katika makabidhiano haya ya kihistoria tunaadhimisha ununuzi wa bidhaa za afya ya uzazi ulofanywa na UNFPA kufikia thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 4.6 kwa Mwaka huu wa 2022 ambapo zaidi ya Dola milioni 4 zinazotoka kwa ugavi wa UNFPA na zaidi ya dola 500,000 zinatoka ofisi ya Maendeleo ya kimataifa na Jumuiya ya Madola ya Uingereza “amesema Schreiner.
Sanjari na hayo Mkurugenzi Ofisi ya Maendeleo ya Uingereza, kimataifa na Jumuiya ya Madola Bi Kemi Williams amesema kwa kutembelea bohari ya dawa amejenga uelewa pia wamethibitisha uwepo wa dawa katika stoo.
Vilevile Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya dawa MSD Ndugu Mavere Ali Tukai amesema UNFPA itasaidia kwenye ununuzi wa dawa na vifaa tiba kuhakikisha zinafika nchini kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.
“Kwa ujumla makabidiano haya ya dawa na vifaa tiba ni muhimu sana na tutahakikisha zinahifadhiwa ili kutatua changamoto ya mama na mtoto” amesema Mavere.