Home Kitaifa CCM Mwanza yasema imejipanga ushindi wa kishindo Mwakani

CCM Mwanza yasema imejipanga ushindi wa kishindo Mwakani

CHAMA cha Mapinduzi mkoani Mwanza kimesema kimejipanga vizuri kuibuka kidedea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 kutokana na mafanikio ambayo yameonekana katika nyanja zote.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Omary Mtuwa akisema kuwa kwa vile utekelezaji wa ilani ya uchaguzi imefanywa kwa kiasi kikubwa hivyo hakutakuwa na shida yoyote.

Alisema wanakusudia kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi kuanzia ngazi ya vitongoji, mitaa na vijiji kwa kiasi kikubwa na hivyo kuendelea kuwa tumaini kwa watanzania.

“Chama chetu hakitasita kumchukulia hatua kiongozi yeyote atakayekuwa ni kikwazo cha utekelezaji wa ilani ya chama chetu kwa maslahi yake binafsi” alisema Mtuwa.

Mtuwa aliwaasa viongozi wote kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa kuwaeleza wananchi wapi na sehemu gani serikali yao imefanya vizuri ili waweze kuendelea kukiamini chama hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!