Home Kitaifa OJADACT yaipongeza Serikali kwa kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya

OJADACT yaipongeza Serikali kwa kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kuliga Vita Matukizi ya Dawa za kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kimeipongeza Serikali kwa kuimarusha Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) kwa kufanya kazi ya kupambana na dawa za kulevya kwa weledi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa OJADACT Bwana Edwin Soko Jijini Arusha kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani.

Bwana Soko amesema kuwa, DCEA imekuwa ikifanya kazi kubwa kwenye mpambano ya dawa za kulevya na kufanikiwa kukamata watuhukiwa wengi wa dawa za kulevya.

Kwa sasa DCEA umekuwa ikifanya kazi kwa weledi sana pamoja kuwaunganisha wadau wa mapambano ya dawa za kulevya pamoja , hii imesaidia kupunguza uingizwaji na usambazaji wa dawa za kulevya Nchini.

OJADACT pia imewashukuru wadau wake mbalimbali wanaofanya nao kazi wakiweno NSSF Mkoa wa Mwanza ambao wote wamekuwa mstari wa mbele kwenye kuisaidia OJADACT kufanikisha shughuli zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!