Home Kitaifa KANISA LAZUNGUSHIA UZIO ZAHANATI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

KANISA LAZUNGUSHIA UZIO ZAHANATI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

Na Shomari Binda- Musoma

KANISA la New Life Gospel Community Church (NLGCC) maarufi kama “Bonde la Baraka” lenye makao makuu mjini Musoma, limeunga mkono juhudi za serikali kwa huduma za jamii.

Huduma iliyotolewa na Kanisa hilo ni kuzungushia uzio zahanati ya Kigera iliyopo manispaa ya Musoma iliyoghalimu zaidi ya milioni 23.

Akizungumza na Mzawa, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Daniel Ouma amesema waliomba kibali kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Musoma kuifanya kazi na imekamilika.

Amesema kama Kanisa wanalo jukumu la kushiriki masuala ya kijamii na hilo walilolifanya ni moja ya jambo muhimu.

Askofu huyo amesema kumekuwepo na baadhi ya watu kuvamia maeneo ya serikali ya kutolea huduma bila kuona umuhimu wake hivyo wameamua kuyalinda kwa kuzungushia uzio.

Dao amesema huduma za afya ni jambo la msingi hivyo maeneo yake lazima yawe na uangalizi mzuri na uzio huo utasaidia.

“Kama Kanisa tumeona umuhimu wa kufanya hivi na tunamshukuru Mungu kwa kukamilisha zoezi hili ambalo tunataraji kukabidhi kazi hii kwa serikali hivi karibuni”

Haya ni matoleo ya waumini Kanisani na sio Kanisa kuwa watu wa kuomba tu wakati mwingine yatupasa kutoa kwenye jamii”, amesema Askofu Dao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa ya Musoma,Bosco Ndunguru, amelishukuru Kanisa hilo kwa jambo muhimu na kubwa walilolifanya

Amesema jamii nyingine inapaswa kuwa ni watu wa kujitoa kufanya mambo ambayo yatasaidia kwenye jamii husika

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!