Home Kitaifa TANTRADE YAPOKEA VIZIMBA VYA MABANDA YA KISASA KWA AJILI YA MAONESHO YA...

TANTRADE YAPOKEA VIZIMBA VYA MABANDA YA KISASA KWA AJILI YA MAONESHO YA 47 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa Khamis leo tarehe 22 Juni, 2023 amepokea udhamini wa Viti, Meza na Vizimba 170 vya mabanda ya Maonesho vyenye thamani ya Shilingi Milioni 300 kutoka kwa kampuni ya manunuzi ya Nchini chini ya East Africa Commercial and Logistic Center ambao pia ni wadhamini wakuu wa Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba).

Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis amesema TanTrade imewaza kuokoa fedha zaidi ya Shilingi milioni 100 zilizokuwa zinatumika kukodisha vifaa hivyo ili kukidhi mahitaji ya Washiriki katika Maonesho hayo.

Nae Meneja Mkuu wa East Africa Commercial and Logistic Center (EACLC) Bi.Wang Xiangyu amesema wanafuraha kuwa wadhamini Wakuu wa Maonesho ya 47 ya DITF, 2023 na hiyo ni hatua ya mwanzo wa ushirikiano kati ya TanTrade na kampuni hiyo na amewakaribisha Watembeleaji kutembelea banda kubwa la Nchi ya China (China Pavellion) linaloratibiwa na kampuni hiyo lililopo kwenye Maonesho ya SabaSaba lenye ushiriki wa Makampuni zaidi ya 50 ya Sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tehema, Mashine na Viwanda, Miundombinu kutoka Nchini China.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!