Home Kitaifa MBUNGE AGNESS AMUOMBA RAIS SAMIA MADAKTARI NA WAUGUZI

MBUNGE AGNESS AMUOMBA RAIS SAMIA MADAKTARI NA WAUGUZI

Na Shomari Binda

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara,Agness Marwa,amemuomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuongeza idadi ya madaktari na wauguzi ili kuwahudumia wananchi.

Hayo ameyasema leo bungeni wakati akizungumza na kipindi cha bunge redio katika shughuli mbalimbali zinazoendelea mkoa wa Mara.

Amesema mkoa wa Mara wanamshukuru sana Rais Samia kwa ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na hospital vilivyo kwa sasa.

Agness amesema kwa sasa kinachohitajika in madaktari na wauguzi wa kutosha ili wananchi wazipate huduma za afya za uhakika.

Katika suala la vifaa tiba na dawa amesema ni muhimu kuwepo kwenye maeneo hayo ya huduma ili adhima ya kutoa huduma iweze kufanikiwa.

Amesema huduma za magari ya wagonjwa na huduma nyingine yanahitajika na kudai kwa kuwa serikali ya Rais Samia ni sikivu kupitia Wizara ya Afya italifanyia kazi

Akizungumzia huduma za maji mkoani Mara,mbunge Agness amesema wanaendelea kumshukuru Rais Samia kwa miradi mingi ya maji iliyopo.

Amesema katika miradi iliyokamilika na inayoendelea dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani itakwenda kukamilika kwa asilimia mia moja

Pamoja na mambo mengine amezungumzia pia masuala ya maadili amewaomba viongozi wa dini kuendelea kukemea vitendo viovu na kudai kwa sasa vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoa wa Mara vimepungua kutokana na wananchi wake kujituma na ujasiliamali

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!