Home Kitaifa WADAU KUUNGA MKONO SERIKALI KUTOA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA YA KISASA

WADAU KUUNGA MKONO SERIKALI KUTOA MAFUNZO YA TEKNOLOJIA YA KISASA

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Tume ya Tehama ICT imesema itaendelea kufanya kazi kubwa kuhakikisha inapeleka huduma za mawasiliano nchi nzima ili kusaidia kujenga uchumi wa kidigital .

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TEHAMA Nkundwe Mwasaga aliopowatembelea wadau waloojitolea kuanzisha kituo cha mafunzo ya teknokojia ya kisasa Punjani charitable trust kwa kushirikiana na Rikiana khoja Leadership forum ambapo amesema wadau hao wanatoa pia na ufadhili(scourlaship)

Hata hivyo amesema kuwapa watanzania wote ujuzi ni kazi kubwa sana hivyo anashukuru kwa kuona wadau mbalimbali wakijitokeza kutoa fursa kwa Vijana katika teknolojia hivyo kwa kutambua hilo serikali ina kanzi data wale wote watakaosomea hapo wataomba majina yao ili wayaweke kwenye mfumo idadi Yao ifahamike Ili kama kutakuwa na uhitaji watumiwe wao .

Kufuatilia Mabadiliko ya kidigital hivyo hatuna budi mifumo yetu ya teknolojia lazima iwe salama ikiwemo ya kifedha na watu wasipoteze hela kwani Vijana wanapokuwa wengi wanafahamu vizuri Teknolojia wanasadia kudhibiti upotevu wa fedha hata wageni wanapokuja waamini nchine yetu ni sehemu salama”amesema Nkundwa

Naye Mwanzilishi wa foundation Punjani Galam Punjani amesema wataahakikisha mafunzo wanayoyatoa kwa vijana wa kitanzania yanaleta tija katika matumizi ya Sayansi na teknolojia katika shughuli zao za kila siku za kiuchumi .

Kwa upande wake Mwanzilishi wa foundation Khoja Leadership forum Dkt Riyaz Hassanalt amesema Tanzania ni nchi ya pekee ina raslimali za kutosha na inakwenda kazi kiuchumi hivyo Vijana wao wakipata fursa ya kuijua teknilojia zaidi watafanya bunifu nyingi zitakazoleta matokeo chanya ya kimaendeleo.

Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kituo hicho kinachotoa mafunzo ya kisasa ya sayansi na teknolojia Isac Marandu amesema hiyo ni fusra kwa watanzani na wazitumie katika ulimwengu wa sasa kwa kuweka juhudia sana hivyo mafunzo hayo yamekuja muda sahihi ..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!