Na Magrethy Katengu
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) imefanikiwa katika Operesheni hiyo DCEA imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 200.5, bagi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978, bangi mbichi gunia 5465, bagi iliyosindikwa kilogramu 1.5, methamphetamine gramu 531.43, heroin kete 3878, cocaine kete 138 , mililita 3840 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine pamoja na kuteketeza ekari 1093 za mashamba ya bangi
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na Kamishna wa (DECEA) Jenerali Aretas Lyimo operesheni maalumu ya kukamata na kudhibiti dawa za kulevya iliyofanyika katika mikoa ya Arusha,Dar es salaam,Kilimanjaro na Pwani ambayo imefanikiwa kukamata dawa mbalimbali za kulevya na watuhumiwa wa biashara hiyo.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema Operesheni yao Maalumu imebaini mbinu mpya zinazotumiwa na Wafanyabiashara wa dawa za kulevya ambao huwatumia wanawake katika usambazaji wa dawa hizo bila wao kujua ikiwemo kuwapatia vifurushi vya mzigo kupeleka eneo lolote na wao kubeba pasipo kujua wamebeba nini hivyo wakikamatwa wakiwataja waliowapa hurukwa na kujikuta wakiwa katika sintofahamu.
“Nawasisitiza wanawake wote nchini kuwa makini pindi wanapotaka kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na raia ya wakigeni kwani wamekuwa wakitumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kwa ajili ya usafirishaji wa dawa hizo pasipo wao kujua” amesema Kamishna
Hata hivyo amesema Zoezi la kamatakamata ni baada ya DCEA kufanya operesheni katika kipindi cha miezi miwili na wiki tatu ambapo ilibaini kuwa hiyo mojawapo ya mbinu ambayo wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakiitumia kwa ajili ya kusafirisha dawa za kulevya.
hata hivyo ametoa onyo Wanawake kuwa makini kwani hali hiyo inaweza kuwasababisha kuingia katika matatizo makubwa ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria huku wanaume wakiwakana bila huruma kwani duniani utu umepotea mwanadamu hajali yeye anaangalia maslahi yake siyo usalama wa mtu .
”Asilimia kubwa ya dawa tulizozikamata tumezikuta zikiwa kwa wanawake una mkuta mtu mmoja anawanawake zaidi ya wawili mpaka watatu na kuficha dawa za kulevya katika makazi yao huku wao wakipanga nyumba tofauti wanakoishi wapenzi wao” amesema Kamshina Jenerali Lymo.
Aliendelea kueleza kuwa hadi sasa jumla ya Wanawake zaidi 20 wamekamatwa na tayari wapo gerezani kutokana na kukutwa wakiwa wamedhiifadhi dawa hizo ambapo tayari wamefikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea.
”Kifungu cha 15 Cha sheria ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya kinaeleza kwamba Ni kosa kusafirisha dawa za kulevya na mtu yoyote atakayethibitika kutenda kosa atawajibishwa kisheria” amesema Kamshina Jenerali Lymo
Aliongeza kuwa Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha inamaliza tatizo la dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii kutokana na kuwepo kwa madhara makubwa ya kiuchumi na kijamii .
Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho Siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya ambayo kitaifa yatafanyika Juni 25 mwaka huu wenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Mamlaka hiyo inawataarifu watu wote kuwa, Juni 26 Juni kila mwaka, Tanzania huungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani.
Sanjari na hayo lengo la siku hiyo ni kuongeza uelewa wa jamii na kuhamasisha Umma kushiriki katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya huku akifafanua maadhimisho haya kwa mwaka huu kitaifa, yatafanyika kuanzia Juni 23 Juni, hadi Juni 25 2023 jijini Arusha.
“Maadhimisho haya yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za udhibiti zinazofanywa na Mamlaka pamoja na wadau wake katika udhibiti wa dawa za kulevya na utoaji elimu kuhusu tatizo la dawa za kulevya.Mgeni rasmi siku ya kilele tarehe 25 Juni, 2023 ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan”
“Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni “Tuzingatie Utu na Kuboresha Huduma za Kinga na Tiba”. Wananchi wote hususani wakazi wa Arusha na mikoa ya jirani mnakaribishwa kushiriki katika maadhimisho hayo, amesema Kamishina Jenerali Lyimo.