Home Kitaifa TANTRADE NA TANROADS WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UWANJA WA MAONESHO YA SABASABA...

TANTRADE NA TANROADS WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UWANJA WA MAONESHO YA SABASABA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (TanRoads) watahakikiaha Uwanja wa Maonesho wa sabasaba unafanyiwa maboresho kwa kukarabati miundo mbinu ya ndani na nje ili kusaidia kuvitia zaidi.

Akizungumza katika kikao kazi kilichafanyika Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania bi. Latifa M. Khamis, amesema wameamua kushirikiana na Tanroads katika kuboresha miundo mbinu ya Uwanja ili kuchochea mabadiliko makubwa na kuyapa zaidi mvuto maonesho ya mwaka huu pamoja na kuleta urahisi wa kufanya biashara.

Lengo ni kuendelea kuboresha miundombinu ya Maonesho ni kusaidiana kuweka Mazingira kwa mazuri kwa makampuni kuonesha bidhaa kwa Wafanyabiashara pamoja na Watembeleaji na kuvutiwa zaidi na sabasaba ya mwaka huu kuleta matokeo yenye tija” amesema.

Aidha kikao hicho kilihudhuriwa na Wataalam kutoka Tanroads Mhandisi Haruin Rashid Senkuku, Mhandisi Elisony Edward Mweladzi, Mhandisi Raymond Godfrey Maimu pamoja na wajumbe wa mkutano huo kutoka TanTrade.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!