Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema mara baaada ya ujenzi wa Shule na Madarasa katika sekta ya elimu ambao unaendelea katika maeneo mbalimbali Zanzibar atahakikisha Serikali inaajiri walimu takribani 4,000.
Â
Amesema hayo leo Julai 16 wakati akiweka jiwe la msingi wa madarasa 12 yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO-19 Shehia ya Kihinani.