Home Kitaifa SEMINA YA WAPIGA PICHA NA VIDEO YAJADILI NAMNA YA KUTANUA MASOKO YA...

SEMINA YA WAPIGA PICHA NA VIDEO YAJADILI NAMNA YA KUTANUA MASOKO YA KIBIASHARA 

WABOBEZI Wa Tasnia ya Picha na video wajadiliana namna ya kutafuta Masoko ya Kibiashara pamoja na kuunda umoja ambao utasaidia kupatiwa fursa za  mbalimbali .

Akizungumza na Wanahabari Mbezi Garden Hotel Jijini Dar es salaam mara baada ya Kumalizika kwa kongamano la Kwanza lililoandaliwa na Mratibu Rajab Mchatta  kutoka Kampuni ya Big Solutions amesema Kwa mara ya Kwanza kumekuwa na muitikio mzuri hivyo kila mwaka kutakuwa na Kongamano hilo lenye lengo la kukamata fursa za kiuchumi.

“Madhumuni ya Semina hii ilikua ni kuwakutanisha wapiga picha na video wawe na Jukwaa lao ili waweze kubadilishana uzoefu na kujadili namna ambavyo wataweza kufanya kazi kwa ufanisi wakiwa na umoja wao ili serikali iweze kuwasaidia kupitia umoja  huo i waweze kutanua Masoko yao ya Kibiashara.”


Mnapokuwa pamoja mnakuwa na nguvu na ushawishi na kupata fursa na kujitathimini kwa kile mnachokifanya katika jamii hivyo semina hii imetengeneza umoja ,kubadilishana uzoefu ,kukutanisha watu mbalimbali ambao ni wabobezi katika tasnia hiyo.”

Aidha ,Mchata ameongeza kuwa Semina itakuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kutathimini vitu mbalimbali ikiwemo fursa za kibiashara na kutafuta Masoko. 


Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Emmanuel Ishengoma amesema Watu wa Tasnia hiyo ni wajasiriamali hivyo benki hiyo inawajali wajasiriamali katika biashara zao na kuhaidikushirikiana nao bega kwa bega.


Tunajua vifaa vinavyotumika ni vyenye thamani hivyo tunawakaribisha wafike ofisi za benki ya Akiba ili waweze kupata nafasi ya kukopeshwa fedha kwa ajili ya kuongeza ubora kwenye kazi zao,kupatiwa bima kwa ajili ya kulinda vifaa hivyo.”


Nae mnufaika wa Semina hiyo Adel Alex ameeleza Mbali na kuongeza weledi, watoa mada wamegusia vitu mbalimbali ikiwemo maswala ya bima,uwekezaji, usalama kazini .
Fursa ya kujifunza hivyo tunahaidi kuongeza weledi ili kuleta ufanisi katika kazi zetu na kukuza Masoko .”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!