Home Kitaifa TAWA YAPOKEA WATALII ZAIDI YA 5000 WALIOTEMBELEA BUSTANI ZA WANYAMA PORI MAONYESHO...

TAWA YAPOKEA WATALII ZAIDI YA 5000 WALIOTEMBELEA BUSTANI ZA WANYAMA PORI MAONYESHO YA 10 YA BIASHARA TANGA

Na Boniface Gideon, TANGA.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyama pori Tanzania ‘TAWA’ imepokea zaidi ya watalii 5000 kwenye Maonesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga yaliyofungwa Jana Juni 6 na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba huku Mamlaka hiyo
ikiwaomba waandaaji wa maonyesho hayo Biashara na Utalii Tanga ambao ni chemba ya Biashara ‘TCIAA’ kuendelea kuboresha mazingira yatakayosaidia na kuwavutia wafanyabiashara, wawekezaji, taasisi , makumpuni , wajasiriamali mbalimbali na wananchi kwa ujumla na hatimaye kuweza kushiriki kwa wingi maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika viwanja Mwahako.

Mamlaka hiyo ya usimamizi wanyama pori Nchini ilikumbwa na adha ya Hali ngumu ya hewa kutokana na Mvua nyingi kunyesha katika Siku za maonesho Hali iliyosababisha Watalii kutokufikia kiwango Cha juu zaidi

Ombi hilo limetolewa na Afisa mhifadhi mwandamizi kutoka mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama pori Tanzania ‘TAWA’ Proches Rongoma mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonyesho ya 10 biashara na utalii yaliyofanyika kwa siku 10 katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga na mkuu wa mkoa huo Waziri Kindamba June 6, 2023.

Rongoma alisema kuwa idadi ya watalii na wananchi waliojitokeza kuangalia wanamnayama mbalimbali katika bustani iliyopo kwenye viwanja hivyo haikuwa kubwa kama ilivyotarajiwa hii ni kutokana na hali ya hewa ambapo mvua zilinyesha kwa wingi hivyo kupelekea washiriki wengi kushindwa kufika katika maonyesho hayo.

Tuliwaambia waandaaji wa maonyesho ya biashara na utalii ambayo ni chemba ya biashara Tanga kutengeneza mradi wa kudumu ambao utaonekana kama maeneo mengine ya maonyesho, kutengeneza mazingira yote ya maonyesho kila banda ili kuweza kuwavutia watalii na wafanyabiashara wengi zaidi kwa maonyesho yajayo”

Maeneo ya mabanda yajengwe katika namna ambayo yatapauliwa na mabati ili yasiharibike mapema yawe ya kudumu tunategemea kwamba wataweza kuboresha eneo hili hasa kunapokuwa na mvua nyakati zote kwa sababu ukiangalia kwa mwaka huu mvua zimeathiri sana tumekosa watalii wengi zaidi ya vile ambavyo tulitegemea” alisema Rongoma.

Akizungumzia maonyesho hayo ya biashara na utalii ya 10 kufanyika jijini Tanga Afisa huyo alisema kuwa kila mwaka TAWA wamekuwa wakiyaboresha kwa kuongeza wanyama pori na ndege wa aina tofauti tofauti hii ikilenga zaidi kuwavutia watalii wa ndani na hatimaye kutembelea hifadhi mbalimbali zilizopo hapa nchini.

Maonyesho ya mwaka 2023 yamekwenda kwa namna ya tofauti zaidi kwa upande wetu TAWA tuliyaboresha kwa kuwaletea Wanyama pori na ndege wa tofauti tofauti na wananchi waliotembelea maeneo haya na kuwaona wanyama na ndege na wamefurahia kuwaona na hiyo yote ni kwaajili ya kuzitangaza hifadhi za Tanzania” aliongeza.

Kwa upande wake Afisa mhifadhi daraja la pili kutoka Mamlaka ya wanyama pori Tanzania TAWA Veronica Mollel amesema ushiriki wao wa kila mwaka katika maonyesho hayo umekuwa na mchango mkubwa katika kuzitangaza hifadhi za Tanzania ambapo wananchi wengi na wadau wamehamasika na kuweza kuzitembelea mbuga mbalimbali zilizopo.

Ushiriki wetu katika maonyesho haya ya biashara na utalii yanayofanyika kila mwaka hapa jijini Tanga umekuwa na tija sana kwa jamii wananchi wengi wamekuwa wakihamasika ukiangalia asilimia kubwa waliokuwa wanakuja katika maonyesho haya waliokuwa wanakuja kuona wanyama kwahiyo sisi Kama TAWA kuwepo hapa tumehamasisha watalii wengi zaidi kuzitembelea hifadhi na mbunga mbalimbali zilizopo”

Aliongeza kuwa kila mwananchi au taasisi inaturusiwa kujenga vitalu na bustani za kufugia wanyama wa aina tofauti tofauti isipokuwa kwa kufuata sheria ambazo ni pamoja na kuwa na leseni ya biashara eneo lenye vigezo vinavyokidhi.

Yasin Mndeme ambaye ni mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maonyesho hayo pamoja na kufanya utalii wa ndani katika bustani ya wanyama pori na ndege alisema ni kuwaona fahari kwao kuwaona wanyama ambao ni adimu hivyo kuiomba serikali pamoja na waandaaji wa maonyesho hayo kuangalia namna ya kuweza kuongeza siku ikiwezekana kufanyika mara mbili kwa mwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!