Home Kitaifa MUHONGO AWAHIMIZA WANANCHI KUONGEZA KASI KUCHANGIA UJENZI WA SEKONDARI

MUHONGO AWAHIMIZA WANANCHI KUONGEZA KASI KUCHANGIA UJENZI WA SEKONDARI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini,Prof.Sospeter Muhongo,amewataka wananchi wa Kijiji cha Muhoji Kata ya Bugwema kuonheza kasi cha kuchangia ujenzi wa sekondari yao.

Muhongo yupo kwenye ziara ya kuvitembelea vijiji 4 vya jimbo hilo vinavyoendelea na ujenzi wa shule za sekondari pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Akiwa kwenye Kijiji hicho cha Muhoji,amesema wananchi wanapaswa kuongeza kasi ya kuchangia ikiwemo nguvu kazi ili lengo la kufungua shule hiyo januari mwakani liweze kutimia.

Amesema serikali inayo majumu ikiwemo kupeleka walimu kwenye shule hiyo pale itakapokamilika hivyo wananchi wanapaswa kuongeza juhudi.

Mmeanza vizuri kuchangia nami nawaunga mkono kwa kuchangia mifuko ya saruji,mabati pamoja na nondo lakini mnapaswa kuongeza kasi ya kuchangia”

Serikali yetu chini ya Rais mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, itachangia shule hii ikiwa ni pamoja na kutuletea walimu wa kutufundishia watoto wetu pale itakapokamilika”, amesema Muhongo.

Wakizungumza kijijini hapo,wananchi hao wamesema watoto wao wanapata shida kutembea umbali mtefu kwenda shuleni hivyo shule hiyo itakuwa msaada kwao.

Wamesema wanamshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini kwa hamasa anayoitoa ili kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.

Vijiji 4 vinavyoendelea na ujenzi wa shule za sekondari kwaajili ya kufunguliwa januari mwakani licha ya Muhoji vipo pia,Wanyere,Nyasaungu na Kisiwa cha Rukuba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!