Home Kitaifa Bodi ya Pamba kuendelea kutoa Elimu ya kuongeza uzalishaji

Bodi ya Pamba kuendelea kutoa Elimu ya kuongeza uzalishaji

BODI ya Pamba nchini itaendelea kuweka jitihada za kumwezesha mkulima kupata kiasi kikubwa cha mavuno kwenye zao la pamba kuondokana na changamoto zinazowakumba wakulima kutokana na mtikisiko wa bei ya zao hilo katika soko la dunia.

Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Mwita Gachuma alisema hayo jana jijini Mwanza kufuaitia kushuka kwa bei ya zao hilo kwenye soko la dunia hatua iliyowafanya baadhi ya wakulima kuyumba.

Alisema kumwezesha mkulima kupata mavuno makubwa kwenye kilimo cha zao la pamba ndiyo suluhisho kwani anapopata kilo chache ni changamoto panapotokea kuyumba kwa bei ya zao hilo kwenye soko la dunia

Leo hii mathalani wakulima wengi wanapata kilo 200 hadi 300 kwa ekari moja hii haina tija kwa mkulima anapaswa kupata hadi kilo 1000 na zaidi” alisema Gachuma.

Aliwataka wakulima walime pamba kwa kufuata kanuni bora za ulimaji wa pamba ili wapate mavuno mazuri badala ya kuendelea kulima kilimo kisicho na tija ambacho kinakatisha tamaa

Gachuma alisema mwaka huu serikali imeamua kutangaza bei elekezi kuwa ni sh 1060 kwa kilo ya pamba mapema mwezi mei mwanzoni kuzuia walanguzi kununua pamba toka kwa wakulima kwa bei ya chini.

Meneja wa Birchand Oil Mill limited ya jijini Mwanza ambayo wanachakata pamba Salum Hamis alitaka wakulima wapewe elimu juu ya bei ya soko la dunia na kulima kwa kutumia pembejeo nzuri ili waweze kupata mazao mengi kwenye eneo wanalolima

Alisema wanatarajia kununua robota 20,000 hadi 30,000 za pamba katika maeneo wanayonunua katika mikoa Mwanza, Simiyu na Mara katika msimu huu wa ununuzi wa pamba.

Hamis alisema kuwa masuala yote ya kuwezesha kununuliwa kwa zao la pamba katika maeneo ambayo Kampuni hiyo inafanya kazi zimekamilika na ununuzi unaendelea japo bado ni kwa kiasi kidogo.

Alisema kiwanda chao huchakata zao la pamba na kupata pamba nyuzi, mashudu, mbolea na mafuata ambayo yana matumizi mhimu kwa mwanadamu na wanayama hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!