Home Kitaifa ACT WAZALENDO YASHAURI SERIKALI KUSHUSHA GHARAMA YA NISHATI MBADALA

ACT WAZALENDO YASHAURI SERIKALI KUSHUSHA GHARAMA YA NISHATI MBADALA

Na Magrethy Katengu

Chama cha ACT wazalendo kimeishauri serikali kuangalia namna bora ya kusaidia Wananchi wanaoshindwa kumudu gharama za kununua nishati mbadala ikiwemo gesi ili kusaidia uharibufu wa Mazingira.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam Waziri Kivuli chama cha ACT Wazalendo Is-haka Mchinjita wakati akichambua bajeti iliyosomwa Jana Bungeni na Waziri wa Nishati January Makamba wameona katika kutekeleza hilo Serikali imetenga Shilingi bilioni 10 ruzuku ya mitungi ya gesi na vifaa zaidi ya 200,000 Vijijini ili watumie nishati mabadala ya kupikia na kusaidia kupunguza uharibifu wa Mazingira.

Serikali imekuwa kwenye mpango wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia (Clean cooking) ambayo ni rafiki wa Mazingira na afya ya mwanadamu na inakadiriwa kwamba kila mwaka hekari milioni moja ya mita inakatwa kwa matumizi ya mkaa na Kuni na tayati matamko yametolewa yakisisitiza taasisinza umma na binafsi kusitisha matumizi ya kuni na mkaa ifikapo 31 mwaka 2025″ amesema Mchinjita

Sanjari na hayo amesema Serikali ifanyie kazi mapendekezo yanayotolewa bei ya gesi ya Shirika la maendeleo la petroli Tanzania inawezwa kupunguzwa kutoka Dola za Marekani 5.19 hadi 4.359 hiyo itasaidia kupunguza gharama kwani TPDC ingewezekana wenyewe ndiyo mauzo yao yawe chini kuliko Mkampuni mengine

Manjita akizungumzia kuhusu suala la umeme ameshauri Serikali iangalie sana suala hilo kwa jicho la tatu kwani Vijivini maeneo mengi hawajafikiwa na Umeme hivyo wanaishi katika Mazingira magumu na gharama ya kuingiza umeme majumbani mwao hivyo bei iangaliwe ili vijiji vyote vifikiwe na umeme ili kusaidia Shughuli za Kiuchumi zifanyikwe kwa wepesi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!