Home Kitaifa NCHI 5 ZAONGEZEKA KUJISAJILI KUSHIRIKI MAONYESHO YA 47 KIMATAIFA TAN TRADE

NCHI 5 ZAONGEZEKA KUJISAJILI KUSHIRIKI MAONYESHO YA 47 KIMATAIFA TAN TRADE

Na Magrethy Katengu

Idara ya Ukuzaji biashara TanTRADE imesema mpaka sasa katika Maonesho ya biashara ya kimataifa ya 47 nchi 5 zimeongezeka kujisajili katika maonyesho hayo huku jumla ya kampuni zilizojisajili elfu moja mia tatu kumi na saba(1317) za ndani zikiwa elfu Moja miambili na tatu(1203)huku za nje kutoka nchi 14 zikiwa mia moja kumi na nne(114)

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa idara ya ukuzaji biashara TanTrade bw. Fortunatus Mhambe amesema Maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa ya nayotarajiwa kufanyika yatakuwa na maeneo mbalimbali yaliyoboreshwa na programu za kuvuta ambapo mpaka sasa nchi zilizothibitisha kushiriki ni China, Singapore, Syria, Irani, Pakistani, Uturuki, Indonesia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Kenya, Ghana, Rwanda, Algeria,

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Chemba ya Uchimbaji Madini Mhandisi Benjamini Mchwampaka amesema katika Maonyesho hayo ya biashara wataandaa majukwaa ikiwemo kuwakutanisha wadau wa wawekezaji katika uchimbaji Madini na wale wote wanaovutiwa kuwekeza katika sekta ya Madini kujadiliana nao fursa zilizopo nao wawekeze katika sekta hiyo

Naye Mkurugenzi wa Tanzania Kwanza strategists LTD Francis Daud amesema watatumia fursa hiyo ya maonyesho ya sabasaba kutangaza raslimali zilizopo na wanaleta teknolojia mpya ya kutambua mchango makampuni mbalimbali katika kuvutia wawekezaji toka.nje ya nchi.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi kutoka kituo cha Uwekezaji TIC Latifa Kigoda amesema watakuwa na banda katika maonyesho hayo na watakuwa wanapokea wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwa kuwasajili hivyo watakuwa na huduma nzuri zote za kumsaidi muwekezaji

Wajasiriamali kutoka Vijijini, Bertha Kageruka, amesema zaidi ya wanawawake 50 Wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali watashiriki maonesho hayo kwani kinamama wengi waliopo vijijini wamethibitisha ushiriki wao, ambapo pia, wamewezeshwa kwa kupewa elimu namna ya kuboresha bidhaa zao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!