Home Kitaifa UUZAJI DAGAA KWA KUTUMIA MIZANI KUANZA MWEZI JULAI

UUZAJI DAGAA KWA KUTUMIA MIZANI KUANZA MWEZI JULAI

Na Neema Kandoro, Mwanza

Wakala wa Vipimo Mkoani Mwanza (WMA) imesema kuwa mwezi wa saba mwaka huu uuzaji wa dagaa ziwani utafanywa kwa kutumia mizani badala ya matumizi ya vipimo visivyo rasmi ambavyo hupunja watu kwenye mnyororo wa thamani kwenye sekta hiyo.

Wito huo umetolewa Leo jijini Mwanza na wadau wa sekta hiyo katika kikao kazi kilichowakutanisha maafisa vipimo, biashara na maafisa uvuvi kutoka Halmashauri ya Buchosa kwa lengo la kupanga mikakati ya kuanza kutumia mizani kupima dagaa badala ya matumizi ya vipimo visivyo rasmi.

Kaimu Meneja wa WMA Mkoani Mwanza Hilolimus Mahundi aliwataka maafisa uvuvi hao ambao wako karibu na kundi hilo la wavuvi kwenda kutoa elimu juu ya ubora wa matumizi hayo ili mwezi wa saba sehemu zote za uvuvi mkoani hapo kuanza kutumia mizani zilizoidhinishwa na wakala katika biashara hiyo.

Alisema kuwa wao wakala wa vipimo kwa kushirikiana na maafisa uvuvi wataendesha uelimishaji kwa jamii kufahamu umuhimu wa kutumia vipimo kwenye biashara hiyo ili kuwezesha wavuvi na walaji kupata faida kwenye shughuli hiyo.

Upimaji wa bidhaa hiyo kwa kutumia vyombo visivyo rasmi humpunja mvuvi na mnunuzi lakini vilevile halamashauri husika hivyo kuanzia sasa hadi mwezi wa saba elimu iwafikie watu wetu wote” alisema Mahundi.

Afisa Uvuvi wa Kisiwa cha Maisome wilayani Buchosa Franco Mwambaka alisema wataenda kusimamia utekelezaji wa sheria ya vipimo kwenye biashara ya dagaa ili mvuvi na mlaji waweze kunufaika.

Alisema kuwa kutokana na biashara ya dagaa kuendelea kufanywa kwa vipimo visivyo rasmi kama vile ndoo,viroba ama sado humpunja mvuvi, mlaji na halmashauri husika hivyo kutakiwa kutakiwa mabadiliko Ili kuondoa hali hiyo

Naye Afisa uvuvi katika kata ya Bulyaheke Kisiwa cha Kasalazi na Gembale wilayani Buchosa alisema kuwa watatembelea katika maeneo yote ili kuhakikisha kuwa wanatoa elimu kwenye jamii juu ya umuhimu wa kutumia mizani katika uuzaji wa dagaa ili waweze kuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza wito huo wa kisheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!