Home Kitaifa IDARA ZILIZOANZISHWA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI KUHIMARISHWA.

IDARA ZILIZOANZISHWA KATIKA MIKOA NA HALMASHAURI KUHIMARISHWA.

Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Conrad Milinga kwa niaba ya Katibu Mkuu amesema Wizara inashirikiana na Tamisemi kuimarisha Idara za Uwekezaji, Viwanda na Biashara zilizoanzishwa katika kila Mkoa na Halmashauri nchini.

Bwana Milinga ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi Idara za Uwekezaji Viwanda na Biashara wa Mikoa kinachofanyika kuanzia Mei 1 16 – 17, 2023 jijini Dodoma kwa lengo la Kupitia Mwongozo utakaorahisisha utendaji kazi na majukumu yao kwenye ngazi ya Halmashauri na Mkoa .

Bwana Milinga pia amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji na biashara kwa kuanzisha Idara hizo kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka Mkoa ili kutoa huduma bora na kwa haraka kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini na hivyo kutimiza malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ninyi ni Timu tunayoitegemea muwe vielelezo, mtakuwa na kazi kubwa kwa wafanyabiashara kutoa elimu namna ya kufanya biashara zao kwa ufanisi kujua wapi anapaswa kuanzia kabla ya kusajili biashara zao na kwa kufanya hivyo tutakusanya mapato mengi kwa amani na kujenga mahusiano mema tunaamini hamtatuangusha “Amesema Milinga.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara ,Wizara ya Uwekezaji na Biashara Bw. Sempeho Manongi amesema kuwa lengo la kuwaita watendaji hao ni kuwaelewesha na kuhamasisha uboreshaji wa mazingira wezeshi ya kibiashara uwekezaji na Viwanda, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kutatua changamoto mbalimbali za wafanyabiashara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki hao wamesema kuwa wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuanzisha Idara hiyo ili kazi za uwekezaji, viwanda na biashara ziweze kufanyika kuanzia Wizarani mpaka chini kwani utekelezaji wa chini haukuwa na usimamizi .

Kupitia vikao kama hivi vinatusaidia kuwa na mtazamo mzuri wa kufanya kazi karibu na hawa wafanyabiashara wanaolipa kodi na tunawaahidi Serikali hatuta waangusha “amesema Sangu Deogratias Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma

Nae Beatrice Charles Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mororgoro amesema kuwa muongozo huo unaenda kufanya kazi kwa uweledi na kwamba wataenda kuondoa vikwazo eneo la uwekezaji na ujenzi wa viwanda itakayosaidia kuongeza mapato.

Lakini pia tutaenda kuimarisha mahusiano kati ya Mikoa, Halmashari, pamoja na Sekta binafsi zilizopo katika maeneo yetu na tutaweka nguvu kwa makundi yote kuwapa ushauri ili wafanye biashara zao vizuri jambo ambalo litasaidia kukuza sekta binafsi. “Amesema Beatrice.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!