Home Kitaifa WATUHUMIWA 125 WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO MBALIMBALI WAKAMATWA JIJINI MWANZA

WATUHUMIWA 125 WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO MBALIMBALI WAKAMATWA JIJINI MWANZA

JESHI la polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watuhumiwa 125 kwa matukio mbalimbali ya kiuhalifu akiwemo mwanachuo mwaka wa kwanza anayesoma kozi ya Famasia Bugando aliyejiteka na kutaka ndugu na marfiki walipe milioni 3.5 ili aachiwe la sivyo atauawa.

Kamanda wa polisi Mkoani Mwanza Wilbroad Mtafungwa aliwaambia wandishi wa Habari jana Jijini Mwanza kuwa matukio hayo yalitokea April 26 ambapo mauaji kwa Imani za kishirikina, matukio ya kujiuza wanawake, ushoga, wizi, uuzaji madawa ya kulevya, mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na mitego ilizuiwa kuwa ni miongoni mwa matukio waliyokuwa wanafanya.

Naomba wananchi wajiepushe na Imani za kishirikina nawasihi tufuate sheria na kuepuka kukatisha maisha ya watu, kufuata sheria na kufuata utamaduni wetu”alisema Mtafungwa.

Kamanda alisema kuwa mnamo Mei 5 walipokea taarifa kutoka kwa Matiko Sirari (29) ambaye ni Daktari wa Hospitali ya Rufaa Kanda Bugando akitaarifu juu ya kutekwa na watu wasiojulikana kwa mwanafunzi wa kozi ya Famasia mwaka wa kwanza aitwaye Kennedy Nyangige (20) na kupelekwa kusikojulikana.

Alisema kwa vile ni tukio la kustaajabisha polisi walianza mara moja msako ili kunusuru maisha ya kijana huyo kwani kwa kutumia simu yake watu wasiojulikana walikuwa wakiwapigia simu watu mbalimbali kuwataka kulipa sh milioni 3.5 ili wamwachie la sivyo wangemua.

Kamanda Mtafungwa alisema polisi walifanikiwa kubaini kijana huyo ambaye alisingizia kutekwa kujihifadhi kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo FM Katapila iliyopo Mtaa wa Igogo wilaya ya Nyamagana akistarehe ndani chumbani kwa kunywa pombe.

Alisema mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa alikiri kutumia simu yake kuwadanganya wazazi, viongozi wa chuo, ndugu na marafiki ili apatiwe fedha kwa ajili ya starehe.

Mtafungwa alisema bado wanamshikilia kijana huyo kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo na kulipatia jeshi hilo kazi ya ziada kunusuru maisha yake na wakati wowote atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake.wa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!