Wananchi wanaoishi kando Kando mwa ziwa Victoria wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya Magonjwa ya kuambukizwa yanayosababishwa na maji ya ziwa na vijito yakiwemo ya Kichocho na minyoo ambayo yamekuwa yakileta madhara Kwa wananchi
Hayo yamebainishwa jana jijini Mwanza na wadau wa sekta ya Maendeleo ya Jamii katika tukio la kutoa elimu, kuwanywesha dawa za minyoo na kichocho watoto waishio katika mazingira magumu kupitia ufadhiri wa Tasisi ya Tanzania Rural Health Movement iliyopo katika Manispaa ya Ilemela.
Mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika Manispaa ya Ilemela Dk Cosmas Balyo alisema kuwa kupitia utafiti waliofanya kati ya watoto 10 waishio katika mazingira magumu tisa wana kichocho.
“Kuvaa viatu,kuosha chakula kwa maji safi kuwa ni njia ya kujikinga dhidi ya magonjwa hayo” alisema Balyo.
Alitoa wito kwa jamii inayoishi kando kando mwa ziwa kuepuka kuoga maji yaliyotuwama kwani madhara yake ni kupata maradhi ya kichocho na minyoo ambayo humsababishia mtu maumivu ya tumbo, kuharisha pamoja na kutokwa damu anapo kojoa.
Meneja Miradi wa Tasisi ya Tanzania Rural Health Movement Augustino Mhanga alisema kuwa wamekuwa wakiwasaidia watoto pamoja na wazee wanaoshi katika mazingira magumu mara kwa mara huduma za dawa za minyoo na kichocho ili kuwaepusha dhidi ya magonjwa hayo.
“Watanzania tujiepushe kukabiliwa na magonjwa hayo ambayo yanasahaulika wakati yakiathiri afya ya watu” alisema Mhanga
Aliomba Taasisi za umma na binafsi kuona dhamana ya kusaidia makundi ya watu wanaoishi katika mazingira magumu kukabiliana na matatizo hayo ili kufanya jamii kuwa na afya bora.