Home Kitaifa TMDF NA FAO YAZITAKA NGOs KUWA WADAU WA KUTUMIA MWONGOZO WA HIARI...

TMDF NA FAO YAZITAKA NGOs KUWA WADAU WA KUTUMIA MWONGOZO WA HIARI WA KUPUNGUZA UPOTEVU NA UHARIBIFU WA CHAKULA

Mwandishi wetu
Dar es salaam

Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisberies Development (TMFD) Bwana Edwin Soko amekutana na Afisa na Shirika la chakula na kilimo Duniani Bwana Omar Riego Penaruba toka Rome na kujadili kwa pamoja umuhimu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini Tanzania kutumia mwongozo wa hiari wa kuounguza upotevu na uhalibifu wa chakula Nchini .

Bwana Soko amesema kuwa, kwa kuwa TMFD ipo karibu na vyombo vya habari hivyo itatumia sauti kuhamasisha umuhimu wa mwongozo huo kwenye kupunguza upotevu na uhalifu wa chakula Nchini.

Pia tutahakikisha mashirika yanayofanya kazi katika sekta ya uvuvi yanaufahamu mwongozo huu wa FAO ili yaweze pia kutengeneza mipango mathubuti ya kuhamasisha jamii kuwa wadau wa kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi kwa kutumia mwongozo huu uliotolewa na FAO.” Alisema Soko

Kwa upande wake afisa wa FAO Omar alisema kuwa masharika yasiyo ya Kiserikali ni wadau wakubwa wa uzuiaji wa upotevu wa mazao ya uvuvi Nchini hivyo itakuwa jambo jema kwa TMFD kusaidia mashirika mengine kuufahamu mwongozo huo.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jijini Dar es salaam na TMFD itaanza mara moja kuunadi mwongozo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!