Home Kitaifa DIWANI ASHA AINGIZA WANACHAMA WAPYA 305 ZIARA YA UHAMASISHAJI VIKUNDI

DIWANI ASHA AINGIZA WANACHAMA WAPYA 305 ZIARA YA UHAMASISHAJI VIKUNDI

Na Shomari Binda-Musoma

DIWANI wa viti maalumu manispaa ya Musoma, Asha Muhamed amefanikiwa kuingiza wanachama wapya 305 wa CCM na jumuiya zake kwenye ziara ya uhamasishaji vikundi.

Wanachama hao wamepatikana kwenye Kata 9 kati ya 16 alizozitembelea kwa lengo la kuhamasisha wanawake kujiunga na vikundi vya ujasiliamali.

Asha amewashukuru wanachama hao wapya kwa kujiunga na chama pamoja na jumuiya zake na kudai atazilipia kadi zao na wao wazilipie ada ili kuwa pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana.

Akizungumza na wanawake kwenye Kata za Kamnyonge na Mwisenge kwenye ziara yake inayoendelea amesema licha ya kujiunga na chama na jumuiya upo umuhimu mkubwa wa kujiunga na vikundi vya ujasiliamali.

Akiwa Kata ya Mwisenge amesema wasikubali kuombwa pesa wakati wa usajili kwa kuwa hakuna gharama kubwa kusajili kikundi.

Amesema muda si mrefu serikali itaanza kutoa fedha za asilimia 10 zinazotolewa na halmashauri kwa vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemavu.

Diwani huyo amewataka wanawake wa Kata hizo kujiandaa mapema kwa kufanya ukamilishaji wa vikundi vyao.

Asha ameendelea mmomonyoko wa maadili uliopo kwenye jamii na kuwaomba wanawake kuendelea kuyasimamia vizuri ili kulinda watoto.

Amesema wanafunzi waliopo mashuleni wasiachiwe walimu pekee bali wazazi na walezi licha ya majukumu ya utafutaji malezi pia yaangaliwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!