Home Kitaifa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa viongozi wa dini hapa nchini kuendelea...

Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa viongozi wa dini hapa nchini kuendelea kutoa msaada kwa waumini katika  kumaliza migogoro

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka pamoja na Viongozi wengine wa Serikali na Chama wakishiriki katika Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Christian Ndossa na msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu iliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fredrick Shoo wakati wa Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Christian Ndossa na msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu iliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Christian Ndossa na msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu iliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwapongeza Askofu Christian Ndossa na msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu mara baada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini katika Ibada iliofanyika Kanisa Kuu la KKKT Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fredrick Shoo, Askofu Christian Ndossa na Msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule katika picha ya pamoja na Maaskofu mbalimbali wa KKKT mara baada ya  Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Christian Ndossa na Msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu iliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fredrick Shoo (Kushoto) na Askofu Christian Ndossa wa Dayosisi ya Dodoma mara baada ya Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Christian Ndossa na Msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu iliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiagana na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Christian Ndossa na Msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu iliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa viongozi wa dini hapa nchini kuendelea kutoa msaada kwa waumini katika  kumaliza migogoro hususani ya ndoa na mirathi kwa amani na utii kwa Mungu ili kuepusha ongezeko la mmomonyoko wa maadili unachangiwa na kuvunjika kwa taasisi ya ndoa na matumizi holela ya mitandao ya kijamii.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Christian Ndossa na msaidizi wake Mchungaji Stanley Tabulu iliofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma leo tarehe 07 Mei 2023. Aidha amewasihi waumini wa KKKT na watanzania kwa ujumla kuzingatia miongozo inayotolewa na viongozi wa dini ili kuepuka madhara makubwa yanayotokana na kuporomoka kwa maadili.

Makamu wa Rais amesema athari za mmomonyoko wa maadili zimeanza kuonekana kwa baadhi ya viongozi na waumini wa madhehebu ya dini wanaoenenda kinyume na mafundisho ya kweli ya dini. Ameongeza kwamba kumekuwepo na viongozi wa dini wachache wanaoharibu taswira nzuri ya dini kwa njia ya mafundisho na mienendo yao isiyofaa katika jamii. Amewasisitiza viongozi wa dini kote nchini kujitahidi kumaliza tofauti miongoni mwao wenyewe ikiwemo migogoro ndani ya Makanisa na Misikiti hapa nchini.

Halikadhalika amewahimiza Maaskofu na viongozi wa dini kwa ujumla kuwafundisha waumini na watanzania neno na sheria ya Mungu kwa ujasiri, kuwa sauti ya wanyonge, kukemea unyanyasaji hasa dhidi ya wanawake na watoto, kusisitiza waumini na watanzania kufanya kazi, kuepuka kupata mali kwa njia zisizo halali, kukemea ubadhirifu na rushwa, kuhimiza uzalendo kwa Taifa, utu wema, kutunza mazingira ya nchi pamoja na kufundisha yaliyo kweli bila kupotosha wala kupindisha neno la Mungu.

Kuhusu kushughulikia tuhuma za ubadhirifu katika miradi mikubwa ya kimkakati, Makamu wa Rais amesema Serikali inazifanyia kazi tuhuma hizo pamoja na  kuendelea kudhibiti mianya yote ya ubadhirifu pamoja na kuwasihi  viongozi wa dini kuendelea kupaza sauti za mamlaka ya Kimungu dhidi ya ubadhirifu serikalini na katika taasisi za kidini hapa nchini.

Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa viongozi wote wa dini kuliombea  Taifa ili kuwa na maendeleo jumuishi, amani, utawala wa haki, uhuru wa kweli. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za makusudi na madhubuti za kulinda haki za raia, kuimarisha amani, kukuza demokrasia, kudumisha umoja, uhuru na mshikamano wa Taifa. Amesema Mheshimiwa Rais ameonesha kwa vitendo dhamira yake ya kujenga umoja wa kitaifa hata kushiriki shughuli za vyama vingine vya siasa.

Kwa Upande wake Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick Shoo ametoa wito kwa waumini na watanzania kuhakikisha wanafuata mafundisho na Imani sahihi ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili. Amesema KKKT inapinga vikali ndoa za jinsia moja na maadili yote yasiofaa katika jamii na kukemea tabia za watu wachache kutumia alama zinazotumika na kanisa hilo katika masuala ya uovu.

Askofu Dkt. Shoo ametoa wito kwa serikali na wananchi kwa ujumla kuweka mkazo katika kufuatilia mienendo ya wanafunzi katika vyuo kutokana na wazazi wengi kupeleka malalamiko kanisani ya mabadiliko ya watoto wao. Aidha amesisitiza kuwepo na huduma za ushauri nasaha kwa wale waliokumbwa na jambo la mmomonyoko wa maadili.

Aidha Askofu Dkt. Shoo ametoa rai kwa serikali na wadau kuongeza jitihada katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo kuwekwa mpango endelevu wa uhifadhi wa mazingira. Amewasihi viongozi wa dini na waumini kutambua uhifadhi wa mazingira ni wito wa Mungu na kila anawajibika katika kuulinda uumbaji.

Askofu wa Dayosisi ya Dodoma Christian Ndossa amesema kanisa hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika kulinda na kudumisha amani. Amesema uwepo wa amani umewezesha wananchi kutekeleza majukumu yao ya kimaendeleo pamoja na kupata nafasi ya kumwabudu Mungu kwa amani. Ameongeza kwamba kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma litaendelea kuungana na serikali katika kuhakikisha linatoa huduma sahihi ya neno la Mungu, huduma za Afya, Elimu pamoja na maadili mema kwa jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!