Home Kitaifa SERIKALI: ZOEZI LA UWEKAJI MIPAKA HIFADHI YA SERENGETI LILIKUWA SAHIHI

SERIKALI: ZOEZI LA UWEKAJI MIPAKA HIFADHI YA SERENGETI LILIKUWA SAHIHI

Na Shomari Binda-Tarime

SERIKALI imesema kuwa zoezi la uwekaji wa vigingi vya alama ya mipaka kwenye vijiji Saba vya Wilaya ya Tarime vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara ni utekelezaji wa tangazo la Serikali namba 235 la mwaka 1968. Hivyo hakuna jambo jipya ambalo serikali imeliongeza.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais( Tamisemi) Angela Kairuki,alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo hayo.

Amesema wamefika eneo hilo kufuatia agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, aliyelitoa Bungeni hivi karibuni kupata ukweli wa malalamiko ya nbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara, aliyedai zoezi hilo halikufuata utaratibu.

Kairuki amesema katika uwekaji wa Vigingi hivyo hakuna jambo jipya lililoongezwa isipokuwa serikali imeweka mipaka yake watu wavione na watambue mipaka halisi hata vizazi vijavyo vijue. na hivyo amewataka wananchi kuheshimu sheria kwa kutoingilia katika eneo hilo.

Amewataka wananchi kutambua kuwa vijiji vipo salama na kuwataka wananchi waliolima katika eneo ambalo mipaka hiyo imewekwa watakapovuna mazao yao wasirudie tena kulima ama kufanya shughuli zozote kwani sheria za hifadhi haziruhusu.

Ameongeza kuwa mipango bora ya matumizi ya ardhi ifanywe na wataalam katika maeneo hayo na TANAPA waendelee kujenga mahusiano mema na Wananchi wanaopakana na hifadhi na kwamba serikali kamwe haiwezi kuwaonea Wananchi wake.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewataka wananchi kuheshimu sheria za nchi ikiwemo kutoingiza mifigo yao katika maeneo ya hifadhi kwani ni kosa kisheria.

Masanja amesema serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa wale wanaovunja sheria kwa kuingiza mifugo yao katika maeneo ya hifadhi lengo ni kuhakikisha hifadhi zinatunzwa na kulindwa Kama rasilimali muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Naye Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, ametoa maombi kwa serikali kwamba wananchi wa maeneo hayo wanachangamoto ya maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao hivyo serikali iwasaidie sambamba na GN itafusiriwe na wataalam kwa lugha ya kiswahili waweze kuifahamu kwa urahisi.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee, akitoa taarifa ya zoezi hilo, amesema limefanyika kwa amani na kwamba imeonekana katika zoezi hilo kaya 87 zilikutwa ndani ya hifadhi pamoja na hekta za mashamba 408 huku wananchi wakiomba kuchimbiwa mabwawa na visima.

Meja Suleiman Mzee amesema yapo maombi yaliyotolewa na Wananchi hao ni pamoja na Kuomba wachimbiwe mabwawa na visima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!