Home Michezo WAZIRI DKT. PINDI APOKEA TAARIFA HITILAFU YA UMEME UWANJA WA MKAPA

WAZIRI DKT. PINDI APOKEA TAARIFA HITILAFU YA UMEME UWANJA WA MKAPA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Mei 6, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, amepokea taarifa ya Kamati aliyoiunda kuchunguza tukio la kukatika umeme katika uwanja huo wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Dar es Salaam Young Africa (Yanga) dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri Dkt. Chana amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara Ndg. Saidi Yakubu kufanyia kazi taarifa hiyo ikiwemo kuchukua hatua zinazostahili kulingana na taarifa hiyo.Tukio hilo la kupokea taarifa lilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu,Bw Nicholas Mkapa.

Kamati hiyo imeongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Keneth Boymanda kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ikiwa na Wajumbe kutoka Wakala wa Majengo nchini TBA, na baadhi ya watumishi wa wizara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!