Home Kitaifa MBUNGE MATHAYO AWAOMBEA BODABODA LESENI KWA MAFUNZO YA MAKUNDI

MBUNGE MATHAYO AWAOMBEA BODABODA LESENI KWA MAFUNZO YA MAKUNDI

Na Shomari Binda

MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo,ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani kuona namna bora ya bodaboda kupata leseni za udereva kwa njia rahisi.

Mathayo amesema iwapo waendesha pikipiki hao maarufu kama bodaboda watapata leseni wataacha kusumbuana na kukimbizana na askari wa usalama barabarani.

Akiuliza swali la nyongeza bungeni kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani hii leo,Mathayo aliuliza kama kuna uwezekano wa bodaboda kupewa mafunzo kwa makundi ili waweze kupata leseni.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Jumanne Sagini,amesema Wizara kupitia jeshi la polisi na vyuo vya ufundi ipo tayari kutoa mafunzo hayo kwa namna mbunge huyo alivyouliza.

Amesema njia hiyo ni nzuri na itawafanya bodaboda wengi kujifunza namna bora ya usafirishaji na kuweza kupata leseni.

Sagini amesema kama eneo la mbunge Mathayo wameanzisha mafunzo kwa makundi ni jambo jema na wapo tayari kupatiwa mafunzo.

Naibu Waziri huyo wa Mambo ya Ndani amesema kama kuna maeneo mengine wanaweza kuanzisha vikundi na kupewa mafunzo kwaajili ya kupata leseni za udereva.

Baadhi ya bodaboda mjini Musoma wamesema wanamshukuru mbunge huyo kwa mara kadhaa kuwasemea akiwa bungeni.

Wamesema bodaboda ni kazi kama zilivyo kazi nyingine hivyo wanapaswa kusemewa bungeni kwenye changamoto zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!