Home Kitaifa PROFESA MUHONGO ASHAURI UVUVI WA VIZIMBA KUPATA SAMAKI WA KUTOSHA

PROFESA MUHONGO ASHAURI UVUVI WA VIZIMBA KUPATA SAMAKI WA KUTOSHA

Na Shomari Binda

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini ameshauri Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwekeza zaidi kwenye uvuvi wa vizimba ili kupata samaki wa kutosha.

Ushauri huo ameotoa bungeni wakati akichangia wizara hiyo na kujikita zaidi kutoa ushauri utakaoleta mafanikio.

Katika mchango wake Muhongo amesema suruhisho la ukosefu wa samaki kwenye maziwa makuu ni kuwezesha uvuvi wa vizimba (Aquacarture).

Amesema uvuvi huo una mafanikio makubwa tofauti na uvuvi wa aina nyingine na wapo waliofanikiwa hadi sasa kwa uvuvi huo.

Mbunge huyo amesems uvuvi ukiwezeshwa utaweza kutoa chakula cha kutosha (food security), ajira na kuchangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Taifa .

“Suluhisho la ukosefu wa samaki ndani ya maziwa yetu makuu, ni kuwekeza kwenye uvuvi wa vizimba (aquaculture) kwa kiasi kikubwa na utawasaidia wavuvi wetu”, amesema Muhongo.

Amesema utafiti unapaswa ufanywe kwenye aina mbalimbali za samaki (species of fish) walioko kwenye maziwa makuu ili utafiti huo uweze kusaidia sekta ya uvuvi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!