WAUZAJI wa maduka ya dawa za binadamu kwa jumla jijini Mwanza wamesema wanatekeleza kwa vitendo utoaji wa maslahi kwa wafanyakazi wao ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wateja wao ili kuwezesha watanzania kupata huduma nzuri za kimatibabu.
Wito huo umetolewa jana jijini Mwanza na wafanyabiashara hao kufuatia dhamira ya serikali kuona kuwa wafanyakazi wa serikali na sekta bianafsi wanapata stahiki zao zote zinazotakiwa ikiwa ni njia mojawapo ya kuwapa motisha ya kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kujituma zaidi.
Mkurugenzi wa Ifakara Pharmacy ambao ni wauzaji wa jumla wa madawa ya binadamu Jijini Mwanza Malaki Philipo alisema wao wanazingatia kwa kiwango kikubwa utoaji wa maslahi stahiki kwa wafanyakazi wao ili kuwawezesha kutoa huduma nzuri kwa wateja wao.
Alisema katika kufanikisha azima hiyo wanaomba serikali iendelee kutoa ushirikiano wa kiushauri kwa karibu kwani wao watoaji wa huduma za afya wako kwenye sekta ambayo ni mhimu kwa uhai wa binadamu hapa nchini hivyo ushirikiano ni kitu mhimu.
“Sisi tunafanya kazi kama ambavyo serikali yetu inatutaka kufanya ili kuwezesha pande zote kuwa na mazingira mazuri ya kiutendaji kazi ambayo ni matamanio kwa mwajiri na mfanyakazi” alisema Philipo.
Naye Meneja wa Jeet Paharmacy ya jijini hapa Nestory Mayenga alisema wao wanafanya kazi kwa mjibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kulipa kodi na kuzingatia mikataba ya kazi kama zilivyoabainishwa na Idara ya kazi.
Alisema wafanyakazi wao wote wana mikataba ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwapa likizo, malipo ya ziada kwenye kazi, haki kwa watumishi wanaopata ujauzito ya likizo na kuzingatia utoaji kazi kwa kuzingatia jinsia.
Mayenga alisema kuwa vilevile wao wametoa kazi kwa makundi yote kwenye jamii wakiwemo wasomi na wasio wasomi kulinagana na eneo gani mfanyakazi anafanya huduma hiyo na wote hao wana mikataba mizuri.
Alisema katika utendaji kazi kuna baadhi ya wafanyakazi ambao wanapata matatizo ya kiafya kazini kushindwa kutenda shughuli zao wanaendelea kuwa nao mpaka wapone.