Home Kitaifa DC-MBULU AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI KATIKA NGAZI YA WILAYA.

DC-MBULU AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI KATIKA NGAZI YA WILAYA.

Katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani ambayo uadhimishwa kila tarehe 1 Mei ya kila mwaka,Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James amejumuika na kusherekea siku hii muhimu kwa kupokea matembezi ya mshikamano,kupokea risala ya vyama vya wafanyakazi,na kutoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa kada mbalimbali za wafanyakazi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliohudhuriwa na viongozi,wananchi na wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi, Komred Kheri James amewapongeza wafanyakazi wote kwa kuendelea kuwa nguzo ya maendeleo ya Taifa kwa uzalishaji Mali, uchangiaji wa pato la Taifa,na utoaji wa huduma bora kwa jamii.

Pia Komred Kheri James amewasihi na kuwahimiza watumishi na wafanyakazi kuzingatia nidhamu kazini,kuepuka migogoro na migongano kazini inayoweza kukwamisha huduma,uzalishaji mali,na kuharibu mahusiano bora kazini.

Komred Kheri James amewahikikishia wafanyakazi wa wilaya ya Mbulu kuwa,Serikali ya awamu ya sita Chini ya Uongozi makini wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,itaendelea kama inavyo fanya sasa kusimamia kwa kasi na ufanisi zaidi haki,stahiki na mazingira bora ya kazi ili kuboresha maisha ya wafanyakazi nchini.Aidha Komred Kheri James amewahakikishia viongozi wa vyama vya wafanyakazi ushirikiano wa kutosha katika kusimamia masuala ya wafanyakazi ndani ya wilaya ya Mbulu.

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kwa mwaka 2023, yanaongozwa na kauli mbiu yenye ujumbe usemao;

“Mishahara bora na ajira za staha ni nguzo kwa maendeleo ya wafanyakazi “ Wakati ni sasa.

Maadhimisho ya mei mosi kwa wilaya ya Mbulu yamehudhuriwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi,Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini,wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi,Vyombo vya ulinzi na usalama,Vyama vya siasa pamoja na wananchi.

Kwapamoja, tunaijenga Mbulu yetu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!