Home Kitaifa MUSOMA VIJIJINI YAJIPANGA KUKAMILISHA UJENZI WA SEKONDARI 3 MWAKANI

MUSOMA VIJIJINI YAJIPANGA KUKAMILISHA UJENZI WA SEKONDARI 3 MWAKANI

Na Shomari Binda-Musoma

JIMBO la Musoma vijijini limejipanga kukamilisha ujenzi wa shule 3 za sekondari na kuongeza idadi ya shule hizo ifikapo januari mwakani.

Shule zinazotarajiwa kukamilika mwakani ni za vijijiji vya Muhoji,Wanyere na kisiwa cha Rukuba na kufanya shule za sekondari za serikali ndani ya jimbo hilo kufikia 28 na za binafsi 2.

Hivi sasa wananchi wa Kijiji cha Wanyere wameanza matayarisho ya kusafisha eneo la ujenzi wa shule ya sekondari kwa kuongeza idadi.

Wanafunzi wa Kijiji cha Wanyere chenye vitongoji 6 wanatembea kilometa 36 kwenda na kurudi kwenye shule yao ya Kata hali iliyowalazimu kuongeza shule ya pili.

Kwa kuanza ujenzi huo tayari wananchi wamechangia mchanga roli 6 na mawe roli 7 mara baadq ya kuandaa eneo la ujenzi.

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini,Profesa,Sospeter Muhongo,ameanza kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.

Wadau na wananchi wameombwa kuchangia ujenzi wa shule ili kusaidia kupunguza umbali mrefu kwa wanafunzi kwenda masomoni.

Michango ya ujenzi wa shule hiyo imeombwa kuwasilishwa kwa:-
Mwenyekiti wa Kijiji cha Wanyere kwa namba
+255 787 295 178, au akaunti ya Serikali ya Kijiji Benji ya NMB namba 30302301050, Tawi la Musoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!