Home Kitaifa BODABODA WATAKIWA KUJIANDAA NA MIKOPO YA PIKIPIKI

BODABODA WATAKIWA KUJIANDAA NA MIKOPO YA PIKIPIKI

Na Shomari Binda-Musoma

VIJANA wanaojihusisha na usafirishaji wa pikipiki maarufu”bodaboda”wametakiwa kujipanga kuwezeshwa mikopo ya pikipiki kutoka serikalini ili kujiletea maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Musoma,Dkt.Khalfan Haule,katika mkutano mkuu wa mwaka wa umoja wa waendesha pikipiki Musoma mjini.

Amesema swrikali inatambua na kuthamini kazi zinazofanywa na waendesha pikipiki katika kusaidia jamii kwenye maeneo yao.

Mkuu huyo wa wilaya amesema serikali imesitisha kwa muda utoaji wa mikopo ili kuweka utaratibu mzuri kuwawezesha kupitia umoja na vikundi vyao.

Amesema muda ukifika wataona matunda hayo ya mikopo na kuwataka kuendelea kufanya kazi zao kwa uaminifu kwa kuzingatia sheria zikiwemo za usalama barabarani.

“Niwashukuru kwa kunialika kwenye mkutano huu muhimu lakini pia niwafikishie salamu za mheshimiwa mbunge ambaye tungekuwa nae hapa lakini anamajukumu mengine.

Mbunge ametuwezesha kugharamia ukumbi na kule ofisini kwetu katuwezesha viti na ameahidi kuendelea kuwa nasi lakini kubwa tujiandae na kuwezeshwa mikopo” amesema Haule.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Musoma,Patrick Gumbo,amesema kundi la bodaboda ni kubwa na linafanya kazi nzuri ambayo viongozi wanawaunga mkono na wapo tayari kuwasaidia.

Kaimu mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mara, ASP, Hannington Kitundu,amesema kila msafirishaji anapaswa kuzingatia sheria ikiwemo kuacha kupakia abiria zaidi ya mmoja.

Akisoma risala ya waendesha pikipiki,katibu wa umoja huo wilaya ya Musoma,Shukrani Mtaki,amesema wanao wanachama zaidi ya 10,000 na vituo 70 vya kubeba abiria na wapo tayari kufuata sheria.

Baadhi ya waendesha pikipiki wamesema wapo tayari kufuata sheria na kuzingatia taratibu zote zikiwemo za usalama barabarani.

Wamesema katika suala la kuwezeshwa mikopo wamefuata taratibu zote lakini bado hawajaweza kufanikiwa kutoka na changamoto kutoka kwa watoaji mikopo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!