Home Kitaifa MAWAKILI WAJIPANGA KUHARAKISHA UTETEZI KATIKA KESI ZAO

MAWAKILI WAJIPANGA KUHARAKISHA UTETEZI KATIKA KESI ZAO

MAWAKILI Jijini Mwanza wameitaka jamii kutoa ushirikiano mapema kwa mashauri wanayoleta kwao ili kuwezesha kupatikana kwa ufumbuzi haraka na hivyo kuweza kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa leo Jijini hapa na baadhi ya Mawakili kwa kufuatia adhima ya Idara ya Mahakama kutaka kuwepo kwa umalizaji wa kesi haraka ili kuwezesha wananchi kuendelea na shughuli zao mapema.

Mawakili hao ambao ni wa kujitegemea wameitaka jamii na serikali kuelewa kuwa wao huwa hawana maslahi ya upande wowote wa kesi yoyote bali huwakilisha utetezi wao ambao Mamlaka ya Mahakama hupima na kutoa haki kutokana na matakwa ya kisheria.

Wakili kutoka Kampuni ya Integral Advocates Gibson Ishengoma ya Jijini hapa alisema kuwa watu wanaofungua kesi hawana budi kutoa ushirikiano wa ushahidi wanapotakiwa kwa haraka ili kuwezesha kufikiwa kwa adhima hiyo ya watu kupata haki zao mapema na hivyo kufanya mambo yao.

Alisema wao kama mawakili hufurahia wanapopata watu ambao wanawapatia ushirikiano mapema ili kuwezesha kumaliza kesi zao mapema kuwawezesha kwenda kufanya kazi zao kwa haraka.

Kuna dhana potofu kwa baadhi ya wateja ambao hufikiria kuwa wanapoleta mashitaka kwa mawakili lazima washinde hiyo si kweli Mahakama hupima upande upi una haki” alisema wakili huyo msomi Ishengoma.

Hivi karibuni Idara ya Mahakama ilielezea dhamira yake ya kuona kesi zinazofunguliwa zinakamilika mapema kuondoa adha ya watu kuchelewa kupata haki pale wanapokuwa wamefungua mahakamani.

Mawakili hao walielezea walivojiandaa kumaliza kutoa utetezi mapema kuwezesha Idara ya Mahakama kutoa hukumu mapema ili kuwezesha watanzania kuendelea na kazi zao mapema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!