Home Kitaifa WAZIRI NDALICHAKO AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU...

WAZIRI NDALICHAKO AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Mtwara wakati akikagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2023 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako wan ne kutoka (kulia) akifuatilia vijana wa Halaiki wakati akikagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa Mwaka 2023 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, leo Machi 31, 2023. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Mwita, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt, Islam Seif na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Prof. Jamal Katundu wa tano kutoka (kulia).
Sehemu ya vijana wa Halaiki wakiwa katika mazoezi kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara leo tarehe 31 Machi, 2023.
Mkufunzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Mswadiku (kulia) akifafanua jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Mwita (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed wakati wakikagua maandalizi katika uwanja huo.

Na: OWM – KVAU – MTWARA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ametembelea na kukagua maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara.

Akiwa katika ukaguzi huo, Waziri Ndalichako aliambatana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Mwita, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt, Islam Seif, Katibu Mkuu wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Rajab pamoja na viongozi mbalimbali katika mkoa huo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Ahmed amewataka Wananchi wa Mtwara na mikoa ya karibu kujitokeza kwa wingi Aprili Mosi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona ili kuungana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!